0

Mkuu wa wilaya ya Liwale bwana Ephrahim Mmbaga jana alifanya ziara ya kukagua shughuli za uzarishaji mali katika sekta ya kilimo hasa katika zao la korosho, katika ziara yake alitembelea katika Shamba la mikorosho la shekhe mkuu wa Wilaya hiyo ndugu Adam Mperengana ambalo ambalo linaukubwa  wa hekali 39.
  mkuu wa wilaya amefurahishwa na upandaji wa mikorosho hiyo kitalaamu hali ambayo mwenye shamba humuwezesha kupanda mazao mengine kama vile mahindi, mihogo na kunde ili kukwepa kilimo cha kuhamahama.
Pia shekhe mkuu alisema msimu huu ukienda vizuri huenda akapata  korosho si chini ya gunia 100.
Mkuu wa wilaya katika ziara hiyo alifuatana na madiwani bi Mnoche na mhe. Myau wote wa kata ya Nangando na mzee Mohamed Mpoto ambaye ni mwenyekiti wa Rifa asasi inayojishughulisha na kilimo Wilayani hapa. 
Bwana Mmbaga amewashauri viongozi wengine wa sekta mbalimbali kuiga mfano huo wa kutumia muda wao vizuri katika shughuli za kuzalisha mali ili kujiletea maendeleo kwa familia zao na hadi Taifa.

Post a Comment

 
Top