0

Mkuu wa wilaya ya Liwale mhe Ephrahim Mmbaga pamoja na kamati ya ulinzi na usalama na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya mhe Abasi Matulilo,na mwenyekiti wa chama cha waendesha bodabodo jana wamefanya mkutano  na wananchi wa kata ya Nangano,lengo kuu la mkutano huo ni kuongea na wananchi juu ya hali ya ulinzi na usalaama katika wilaya yetu.

Pamoja na hayo mkuu wa wilaya aliwapa mkono wa pongezi kwa vijana wapatao 8 wa familia moja ya mzee Ndembo kwa kuonesha kwa vitendo ile kauli ya ulinzi shirikishi ambao aliwakabidhi kila mmoja wapo bahasha yenye pesa  elfu hamsini kwa juhudi zao za kufanyikisha kumkamata bwana Issa Mfaume ambaye ni mtuhumiwa  wa mauaji aliyoyafanya tarehe 19/09/ 2014 kwa kijana  Zalali Lunje akiwa kwenye mziki katika ukumbi wa Sanabu club kwa kumchomwa kisu kwa sababu zisizojulikana na kusababishia kifo hapo hapo na kijana huyo baada ya kufanya mauaji hayo alitokomea kusikojulikana hali ambayo ilileta wasiwasi kwa wakazi wa liwale nakupelekea kusitisha kufanya shughuli zao za uzarishaji kama kwenda shamba nk wakihofia kukutana nae na huenda akawajelui pia.

Baada ya kutokea tukio msako mkali ulianza kumtafuta ili kurejesha hali ya amani hapa wilayani,bahati nzuri vijana 8 niliowataja hapo juu wa kata ya Nangano walikaa usiku kucha kwenye barabara ya Liwale kwenda Nachingwea kwa lengo la kutimiza wajibu wa ulinzi shirikishi hatimae tarehe 21 kuamikia tarehe 22 mtuhumiwa alikamatwa,mtuhumiwa huyo akiwa njiani anapelekwa kituo cha polisi cha wilayani Liwale alipofika maeneo ya stendi kuu ya Liwale wananchi wenye hasira kali walimvamia na kumpiga mawe na kumkakatakata na mapanga hadi kufa kisha mwili wake wakauchoma moto hali iliyoleta tena taharuki kubwa katika jamii.

Mkuu wa wilaya kama kiongozi wa serkali ameiasa jamii kutokujichukulia sheria mkononi badala yake wanapomtuhumu mtu katenda kosa wamfikishe kwenye vyombo vya dola ambavyo vina dhamana ya kufanya kazi yake na hatimae sheria kufata mkondo wake.

Post a Comment

 
Top