Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe, akifurahi na Watoto Yatima na Waishio katika Mazingira
Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi kabla ya
kufuturu nao futari maalum aliyoiandaa kwa ajili ya watoto hao zaidi ya
80 ambao wanalelewa katika kituo hicho.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (kushoto), akijiandaa kufuturu na Watoto Yatima na
Waishio katika Mazingira Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini Nachingwea
mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliandaa futari maalum kwa ajili ya watoto
hao zaidi ya 80 ambao wanalelewa katika kituo hicho.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (katikati), akizungumza jambo na Shekhe Mkuu wa Wilaya
ya Nachingwea, Abdul Mpakate (watatu kulia) wakati wa kufuturu futari
maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya Watoto Yatima na Waishio katika
Mazingira Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi.
Waziri Chikawe aliandaa futari hiyo kwa watoto zaidi ya 80 wanaolelewa
katika kituo hicho.
Shekhe
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Abdul Mpakate akitoa dua la kumshukuru
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), kwa kuandaa futari maalum kwa
ajili ya Watoto Yatima na Waishio katika Mazingira Hatarishi wa Kituo
cha Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliandaa futari
hiyo kwa watoto zaidi ya 80 wanaolelewa katika kituo hicho. Picha zote
na Felix Mwagara.
Post a Comment