Mgeni rasmi Meneja Sheria wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)Taifa,Abrahamu
Siyovelwa akizungumza na wahitimu katika mahafali ya chuo cha Mutco
yaliyofanyika mwishoni mwa wiki. (picha zote na Denis Mlowe)
Mkuu wa
chuo cha Mutco Leuterius Mheni akisoma taarifa ya chuo mbele ya
wahitimu na wageni waalikwa katika mahafali ya kuhitimu astashahada ya
ualimu chuoni hapo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo hicho.
Na Denis Mlowe,Mufindi
WAHITIMU
mafunzo ya Ualimu katika chuo cha Ualimu Mufindi (MUTCO) kilichoko
wilayani Mufindi mkoani Iringa wametakiwa kutokukurupuka kukopa katika
taasisi mbalimbali za mikopo zinazowafata mara baada ya kupata ajira kwa
kuwa zinamalengo ya kuwafanya kuwa maskini na kuishi kwa kukopa na
kulipa.
Kauli
hiyo imetolewa na Meneja Sheria wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa
Umma (PSPF) Taifa,Abrahamu Siyovelwa , aliyekuwa mgeni rasmi katika
mahafali ya tatu katika chuo yaliyofanyika mwisho mwa wiki katika ukumbi
wa MUTCO, alisema badala yake wafanye chaguo sahihi wakati wa kukopa na
kuangalia na kupitia mikataba kabla ya kujiunga na kuchukua mikopa
katika taasisi hizo.
Siyovelwa
alisema kuwa ni vema watumishi wanaoingia katika ajira mpya
kutokukurupuka pindi wanapotaka kukopa katika taasisi mbalimbali za
kifedha kwa kuwa baadhi ya tasisi hizo zimejawa na ujanja ujanja katika
mikataba yao.
“Naowamba
sana kuwa makini sana katika kukopa hivyo ni wakati wa watumishi wapya
hususani walimu kufanya chaguo sahihi katika kukopa mtaishi maisha ya
kukopa na kulipa hadi mwisho wa kuustaafu kazi na kutolea mfano ukitaka
kujua unakokwenda angalia umbali wa ulikotoka hivyo kuwenu makini sana
na baadhi ya taasisi ” alisema Siyovelwa
Aliwataka
wahitimu hao kutumia changamoto zilizoko katika mazingira watayopangiwa
kuzitumia kama fursa katika kujiletea maendeleo hasa kwa walimu
watakaopangiwa sehemu ambazo huduma za jamii ni chache na kuzitumia
kuwekeza na kuacha kukimbia changamoto hizo
Aidha
aliwaasa wahitimu hao kujiunga na PSPF kwa kuwa kuna baadhi ya mafao
mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo yanalenga kuwawezesha watumishi
kukabilina na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utumishi wao
kabla na baada ya kustaafu
Siyovelwa
alisema PSPF ina mpango imeweka mahususi wa kuhakikisha unaboresha
maisha wa wanachama wake wakiwemo walimu hivyo kuwataka kuwekeza kwa
faida ya maisha yao.
Katika
mahafali hayo mfuko huo wa PSPF umechangia mabati 100 yenye thamani ya
sh. Milioni 1.8 kwa chuo hicho kwa lengo la kukamilisha baadhi ya
majengo ya chuo hicho ambayo hayajakamilika.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo hicho Leuterius Mheni amesema kuwa chuo hicho
kilianza rasmi mwa 2010 na jumla ya wahitimu 64 kati ya wahitimu 76 wa
cheti cha astashahada.
Alisema
chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo huduma ya maji
na vifaa vya kufundishia, ambapo uongozi wa chuo umekuwa likifanyia
jitihada za kuzitatua mara pesa inapopatikana.
Katika
risala yao wahitimu wamesema kuwa ualimu sio jalala la watu walioshindwa
hivyo wameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kutoa
mtaala mpya utakaosaidia ubora wa elimu nchini kwa kuchukua walimu wenye
sifa na waliosomea mafunzo ya ualimu.
Post a Comment