Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta Kebwe Stephen Kebwe amelieleza
Bunge kuwa Wizara imeandaa mpango wa kukabiliana na ugonjwa wa Homa ya
Dengue uliosababisha vifo vya watu watatu kuanzia Januari mpaka mwezi
huu ikiwa ni pamoja na kutenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya ugonjwa
huo.
Mheshimiwa Kebwa amesema tangu ugonjwa huo ugundulike nchini, wagonjwa waliothibishwa kuugua ugonjwa huo ni 450 na kati ya hao wagonjwa wapya 60 wamegundulika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na jitihada mbalimbali za serikali za kupambana na ugonjwa huo kama
kutoa elimu kwa wananchi Timu ya Taifa ya maafa kukutana marambili
kwa wiki ili kutathimini mikakati ya dharura naibu waziri huyo
amewataka watanzania kutokuwa na hofu,kwani auambukizwi kwa kumuhudumia
mgonjwa au kumugusa.
Post a Comment