0

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Ufuluma wilaya ya Uyui  ambapo aliwaambia wananchi hao Kilimo cha Tumbaku kiondoe umasikini na si kuongeza umasikini kwa mkulima.

Wakulima wa Tumbaku kata ya Ufuluma wamelalamikia kulazimishwa na viongozi wa vyama vya ushirika kuuza tumbaku yao katika vyama hivyo ,hata kama sio wanachama.Kinana amewataka wakulima hao kutokukubali kusumbuliwa kuuza tumbaku yao katika vyama hivyo ambavyo baadhi yake vimejaa walaghai na wanyonyaji wa wakulima hao.

Amesema kuwa Wakulima wa zao hilo la tumbaku wamekuwa wakifanya kazi kubwa na ngumu,lakini hawafaidika na jasho la kazi yao,kutokana na kuanzishwa kwa vyama vingi vya ushirika ambavyo vipo kwa faida ya wajanja wachache,hivyo wakulima hao wasilazimishwe kuuza tumbaku yao kwa vyama vya ushirika.ae Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh Fatma Mwasa aliongeza kuwa mnamo mwaka 2012 wakulima wa Tumbaku waliibiwa kiasi cha fedha shilingi Bilioni 16,kama vile haitoshi mnamo mwaka 2013 wakulima hao waliibiwa kiasi cha fedha shilingi bilioni 12 na umoja wa vyama vya ushirika,akabainisha kuwa kufuatia ubadhilifu huo mkubwa wa fedha kwa wakulima,mwaka huu tumbaku haitatolewa kienyeji kwa vyama hivyo mpaka wahakikishiwe fedha zao zitalipwaje.


Akabainisha kuwa imefika wakati wakulima wa Tumbaku wajitegee,wawe huru na kuamua ni wapi wauze tumbaku yao na kwa bei waitakayo ni si kupangiwa na vyama vya ushirika,akaongeza kwa kusema kuwa Wakulima hao wasilazimishwe kuuza tumbaku yao kwa Vyama vya ushirika. 

Kinana amemaliza ziara yake wilayani Uyui leo  na kesho ataunguruma wilayani Sikonge mkoani Tabora. 
 Wakazi wa Ufuluma wakishangilia na wengine wakifuatilia jambo kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye kata hiyo ya Ufuluma,wilayani Uyui mkoani Tabora. 
Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini Ndugu Shaffin Mamlo Sumar akihutubia wakazi wa kata ya Ufuluma kwenye mkutano wa CCM uliofanyika Ufuluma,wilayani Uyui mkoani Tabora.
 Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Ufuluma mapema leo jioni katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora.
 Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Uyui,Mussa Ntimizi akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Ufuluma,Wilayani Uyui mkoani Tabora.
Ads by OnlineBrowserAdvertisingAd Options
 Sehemu ya baadhi ya Walimu kutoka sehemu mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao jioni ya leo mkoani Tabora
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana  akizungumza na Sehemu ya baadhi ya Walimu kutoka sehemu mbalimbali mkoani Tabora jioni ya leo,ambapo Walimu waliwasilisha changamoto zao mbalimbali,na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliyajibu papo kwa papo na mengine aliahidi kuyafanyia kazi na mengine aliyapatia majibu mapema iwezekanavyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Uyui,Mh Lucy Mayenga wakijiandaa kuingia kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
  Mkuu wa Wilaya ya Uyui,Mh Lucy Mayenga akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye Ofisi yake wilayani humo.Kinana amekuwa wilayani humo kwa ziara ya kutekeleza  na kuhimiza Ilani ya CCM,kukagua maendeleo ya Miradi mbalimbali na kusikiliza kero za Wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
  Mkuu wa Wilaya ya Uyui,Mh Lucy Mayenga akizungumza jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo Pichani),kwenye makao Makuu ya wilaya hiyo katika kijiji cha Isikizya mkoani Tabora. 
 Wapiganaji wakiwa kazini
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ,Halmashauri ya wilaya ya Uyui imejenga nyumba nane kwa ajili ya watumishi wake.
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Uyui huku akipokea maelezo ya mradi wa ujenzi kutoka kwa Mhandisi wa Wilaya Ndugu Stephen Nyanda.
 Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mapema leo.
 Kinana akikagua Mradi wa ujenzi wa kituo cha Polisi,wilayani Uyui
 Kinana akipewa maelezo juu ya mradi wa chanzo cha maji,katika kijiji cha Isikizya,wilayani Uyui.



 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiweka kibao cha kumbukumbu kuonyesha mti alioupanda kwenye shule ya sekondari Lolangulu piaKatibu Mkuu alikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara  kwenye sekondari hiyo iliyopo kata ya Ilolangulu wilayani Uyui mkoa wa Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Uyui uliofanyika kata ya Ulolangulu. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akioneshwa moja ya kifaa cha maabara na mwalimu wa Fizikia,Mahugila Chandarua wakati akipita kukagua  maabara ya shule ya sekondari ya Kata ya Ndono,wilaya ya Uyui mkoani Tabora. Katika mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa  Sasa wilaya ya Uyui imekamilisha maabara katika shule za kata tano na zingine sita kukamilishwa mwaka ujao wa fedha.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua ukarabati wa Zahanati ya Ufuluma katika kata ya Ufuluma wilaya ya Uyui,mkoani Tabora 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisomewa taarifa na  Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Tabora Ndugu Erasto Chilambo ,Shirika la Nyumba la Taifa linajenga nyumba 50 katika wilaya ya Uyui.

Post a Comment

 
Top