Mbu aina ya Aedes anayeeneza virusi vya homa ya dengue.
UGONJWA wa
homa ya dengue yaani “dengue fever” umeingia jijini Mwanza ambapo
mgonjwa wa kwanza ameripotiwa kulazwa hospitali ya mkoa, Sekou Toure.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Valentino Bangi amehibitisha kuingia
ugojwa huo ndani ya mkoa wake.
Ugonjwa
huu ulithibitishwa kuingia nchini baada ya sampuli zilizochukuliwa
kutoka kwa watu waliohisiwa kuwa na ugonjwa huo jijini Dar es Salaam
kupelekwa kwenye maabara ya Taifa Dar es Salaam na kuthibitisha kuwa na
virusi vya homa ya dengue mwishoni mwa mwezi wa Januari 2014.
Hadi
sasa idadi ya wagonjwa ambao wamethibishwa kuwa na ugonjwa huo ni 400
na vifo 3. Kwa wiki iliyoshia tarehe 9 Mei 2014 idadi ya wagonjwa
waliogundulika mkoani Dar es Salaam ni 60 (42-Kinondoni, 14-Temeke na
4-Ilala).
Post a Comment