Mwananchi wa Afghanistan akipiga kura ya kumchagua rais mpya wa nchi hiyo.
WANANCHI
wa Afghanistan wamejitokeza kwa wingi jana Jumamosi (Aprili 5, 2014)
kumchagua mtu wa kuchukuwa nafasi ya Rais Hamid Karzai katika
makabidhiano ya kwanza ya madaraka kwa njia ya kidemokrasia wakati
vikosi vinavyoongozwa na Marekani vikikamilisha vita yao vya miaka 13
nchini humo.
Licha ya
vitisho vya kundi hatari la Taliban, upigaji kura kwa kiasi kikubwa
ulifanyika kwa amani huku kukiwa na misururu mirefu katika miji nchini
kote wakati wapiga kura wakipiga kura zao chini ya ulinzi mkali takriban
katika vituo 6,000.
Taliban
imeukataa uchaguzi huo kuwa ni njama za kigeni na imewataka wapiganaji
wake kushambulia wafanyakazi wa uchaguzi, wapiga kura na vikosi vya
usalama.
Mkuu wa
Tume Huru ya Uchaguzi (IEC), Ahmad Yusuf Nuristani ameliambia shirika la
habari la AFP kwamba watu wengi wamejitokeza kupiga kura kuliko vile
ilivyotarajiwa lakini hakutaja idadi bali amesema idadi hiyo ni ndogo
katika maeneo ya vijijini kulinganisha na mijini.
TUNAWATAKIA UCHAGUZI UWE WA HAKI,UHURU NA AMANI
Post a Comment