TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tume
ya Kurekebisha Sheria Tanzania imeanza kufanya utafiti wa mfumo wa
sheria unaosimamia Haki za Walaji ili kubaini kasoro mbalimbali
zilizoko kwenye mfumo husika na kupendekeza njia sahihi ya kuboresha
mfumo huo nchini Tanzania.
Hatua
ya Tume kufanya utafiti huo inatokana na mendeleo ya sayansi,
teknolojia pamoja na utandawazi ambayo kwa ujumla yamemfanya mlaji
kujikuta akiwa kwenye hatari ya kuathirika kiafya, kiuchumi na kijamii.
Tume
katika utafiti wa awali, imebaini kuwa Mfumo uliopo hauendani na na
wakati huu wa mabadiliko ya kiuchumi, kijsamii, kitekenologia
yanayotokea, kwani sheria nyingi zilizopo zilitungwa muda mrefu na hivyo
hazikuzingatia mahitaji ya wakati wa sasa.
Pia
sheria nyingi hazijajumuishwa kwenye sheria moja zinasimamiwa na watu
au Taasisi tofauti tofauti. Hivyo, Tume imeona haja ya kupitia sheria
hizo ili kupendekeza mfumo wa sheria utakaomlinda mlaji kwa kuzingatia
maendeleo yaliyopo sasa.
Na
ni matarajio yetu baada ya kukamilika kwa utafiti huu Tume tutakuja na
mapendekezo ambayo yataleta tija kwa walaji wetu pamoja na taifa kwa
ujumla.
Tume
ya Kurekebisha Sheria (Tume) ilianzishwa chini ya kifungu cha 3 cha
Sheria ya Kurekebisha Sheria Namba 11 ya mwaka 1980. Sheria hii kwa sasa
ni Sura ya 171 ya Sheria za Tanzania Toleo la Mwaka 2002. Tume ya
Kurekebisha Sheria ni Idara ya Serikali inayojitegemea chini ya Wizara
ya Katiba na Sheria.
Imetolewa na;
Tume ya Kurekebisha Sheria (T)
Dar es Salaam
04 Aprili, 2014
Post a Comment