Mahakama
kuu inayoendelea mjini Geita mkoani Geita imemhukumu adhabu ya
kunyongwa hadi kufa Mathias Tangawizi(46) mkazi wa kijiji cha Ibondo
katika kata ya Katoro wilayani Geita baada ya kupatikana na kosa la
kumuua mama mkwe wake aitwaye Sofia Kamuli (51)mwaka 2008.
Akisoma
hukumu hiyo jaji wa mahakama kuu Richard Malima amesema kuwa mtuhumiwa
alitenda kosa hilo tarehe 24 mei 2008 ambapo inadaiwa kuwa mama mkwe
alikuwa anamtaka mtoto wake aachane na mme wake kwani alikuwa na uwezo
mdogo wa kimaisha na baada ya kupata taarifa hizo mtuhumiwa ndipo
alipotenda kosa hilo dhidi ya mama mkwe wake.
Awali mwanasheria wa serikali Emiri Kiria aliiambia mahakama kuwa mnamo tarehe 24 mei 2008 huko katika kijiji jirani
cha Kaduda katika kata ya katoro majira ya saa 3.30 asubuhi mtuhumiwa
alimfuata mama huyo na kumchoma mkuki sehemu za shingoni na tumboni hadi
kufa.
Baada ya kufanya mauaji hayo kwa kuchoma mkuki mama mkwe wakeSofia
Kamuli (51)ambaye alikuwa mkulima,Mathias Tangawizi alimtoa nje
marehemu kwa kumvutia ndani na kufunga milango huku akitokomea
kusikojulikana.
Ameongeza
kuwa baada ya siku mbili mtuhumiwa huyo alikamatwa kwani alikuwa
amerudi katika kijij chake cha Ibondo ndipo jeshi la polisi lilimtia
hatiani kwa kuhusika na mauaji hayo.
Aidha
ushahidi uliotolewa na mashahidi saba kwa mfululizo umekuwa wa
kuridhisha dhidi ya mtuhumiwa ambao haukuwa na mashaka yoyote hivyo na
kuiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo ili liwe fundisho
kwa wengine wenye nia ya kutaka kutenda unyama huo.
Mara
baada ya mahakama kusikiliza pande zote za mtuhumiwa na mlalamikaji
ilijiridhisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo kwa kudhamiria hivyo
mahakama ikaamua kumtia hatiani kwa kunyongwa hadi kufa kwa mujibu wa
kifungu cha 197 sura ya 16 cha mwaka 2002.
Kwa
upande wa mtuhumiwa alijitetea kuwa apunguziwe adhabu kwa amekaa
mahabusu kwa uUda mrefu hivyo angeweza kupunguziwa adhabu vilevile
alijitetea kuwa mara baada ya kuingia mahabusu amekuwa akisumbuliwa na
maradhi mbalimbali hivyo apunguziwe adhabu lakini Mahakama ilitupilia
mbali maombi ya mtuhumiwa huyo.
Na Valence Robert- Geita
Post a Comment