"Ghasia katika maandamano mjini Khartoum ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta"
Wanamageuzi maarufu katika
chama tawala cha Sudan wametangaza kuwa wanatoka chamani kuunda chama
kipya, ishara kuwa mzozo umezidi ndani ya serikali.
Wanaharakati hao wamelalamika juu ya
ukandamizaji wa maandamano ya hivi karibuni ya kupinga kupanda kwa bei
ya mafuta nchini humo.
Piya wamekishutumu chama cha Kiislamu cha National Congress kwamba kinakwenda kinyume na misingi yake.
Kati ya waliotoka ndani ya chama ni aliyekuwa mshauri wa Rais Omar al-Bashir.
Mwandishi wa BBC mjini Khartoum anasema serikali
ya Sudan inapata shida kumudu uchumi unaozidi kuzorota, hasa kwa sababu
ya kukosa pato kutokana na mafuta baada ya Sudan Kusini kujitenga mwaka
wa 2011.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment