Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal na Uhispania Mikel Arteta amekubali kuteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu hiyo ya England. (Goal.com)
Iwapo Arteta, ambaye kwa sasa ni mkufunzi msaidizi Manchester City ataondoka Etihad na kwenda Emirates, Pep Guardiola anapanga kumchukua kiungo wa kati wa zamani wa Barcelona na Uhispania Andres Iniesta, 34, kama mchezaji mkufunzi. (Yahoo)
Kipa wa Manchester City Joe Hart, ambaye aliachwa nje ya kikosi cha England kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia atakuwa anatafutwa na Southampton na Wolves baada ya West Ham kuamua hawamtaki kwa mkataba wa kudumu. Hart, 31, amekuwa West Ham kwa mkopo. (Mirror)
Leicester wanataka kumchukua beki wa Ireland Kaskazini Jonny Evans, 30, kutoka West Brom, lakini huenda ada ya £4m inayodaiwa na wakala wake ikawa kikwazo. (Mail)
Stoke City wanataka aliyekuwa meneja wa West Ham David Moyes awe meneja wao mpya baada ya Paul Lambert kuondoka klabu hiyo iliposhushwa daraja hadi ligi ya Championship. (Sun)
Meneja wa zamani wa Ipswich Mick McCarthy ameambia Stoke wanaochezea uwanja wa Bet 365 kwamba angependa kuwa meneja wao mpya. (Telegraph)
Mkufunzi mkuu wa zamani wa Crystal Palace Frank de Boer na meneja wa Ostersund Graham Potter ndio wanaoongoza katika kinyang'anyiro cha kumrithi Carlos Carvalha Swansea.(Guardian)
Nyota wa Everton Wayne Rooney, 32, anaaminika kuwa kwenye shughuli ya kuamua iwapo akubali ofa kutoka kwa DC United inayocheza Ligi Kuu ya Soka Amerika na Canada (MLS). Nahodha huyo wa zamani wa England amewekewa mlango wazi kurejea Everton wakati wowote akitaka iwapo atakwenda Marekani. (Mail)
Southampton wanapanga kuwasilisha ofa ya £20m kumtaka beki Mwingereza anayechezea Middlesbrough Ben Gibson, 25. (Sun)
Aston Villa wamekuwa wakimfuatilia mshambuliaji wa Mali anayechezea Porto Moussa Marega, 27, wanapojiandaa kwa uwezekano wa kurejea kucheza Ligi Kuu England. (Mirror)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amekiri kwamba huenda akjafutwa kazi iwapo klabu yake itashindwa kulaza Manchester United katika fainali ya Kombe la FA Jumamosi. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Blues na Uhispania Cesc Fabregas, 31, anasema angependa sana kushinda Kombe la FA kupata medali ya kujaza nafasi iliyoachwa na medali aliyoipoteza ya ushindi wa FA akiwa na Arsenal mwaka 2005. (Guardian)
Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri amesisitiza kwamba hajakuwa na shaka kuhusu kusalia katika mabingwa hao wa Italia licha yake kutafutwa na Arsenal na Chelsea. (London Evening Standard)
Arsene Wenger, ambaye anaondoka Arsenal baada ya miaka 22, huenda akaacha ukufunzi na badala yake awe meneja mkuu wa miamba wa Ufaransa Paris St-Germain. (Mirror)
Mkufunzi mkuu wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema kiungo wa kati wa England Ruben-Loftus Cheek, 22, ni miongoni mwa wachezaji wazuri Zaidi aliowahi kufanya kazi nao. (Times)
Kiungo wa zamani wa Newcastle Kenedy, amerejea Chelsea baada ya kuwa kwa mkopo St James' Park, lakini amedokeza kwamba yuko radhi kurejea Newcastle. Mbrazil huyo wa miaka 22 amesema: "Pengine siku moja nitarejea." (Newcastle Chronicle)
Mkufunzi mkuu wa Celtic Brendan Rodgers amesema kwamba bado angefutwa na Liverpool hata kama angefanikiwa kushinda Ligi ya Premia akiwa nao. (Times)
Mashabiki wa Liverpool wametahadharishwa na klabu hiyo dhidi ya kununua tiketi za fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya itakayochezwa 26 Mei kutoka kwa watu ambao hawajaidhinishwa rasmi kuuza tiketi (Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa Stoke na Uhispania Bojan Krkic anasema amekuwa akitatizwa na kuwa na wasiwasi kupita kiasi, lakini "hakuna anayetaka kuzungumzia hilo". (Guardian)
Meneja Chris Wilder anatarajiwa kutia saini mkataba mpya Sheffield United mapema wiki ijayo baada yake kupata hakikisho kutoka wka wamiliki wa klabu hiyo.
Post a Comment