1
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani Liwale mkoani Lindi imemfikisha mahakamani Rashidi Miraji Sogoty ambaye ni kaimu meneja wa mamlaka ya mapato TRA  wilaya ya Liwale kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa.

Kwa mujibu wa vifungu vya sheria kosa hilo ni chini ya kifungu cha 15 ibara ya kwanza a na ibara ya pili cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na ibara ya  11 ya mwaka 2007

Kulingana na uchunguzi uliofanyika imebainika kuwa mnamo tarehe 05.02.2018  Rashidi Miraji Sogoty alipokea hongo ya jumla ya shillingi laki saba (700,000) badala ya shillingi millioni moja na laki mbili alizoziomba kutoka kwa mfanyabiashara mmoja wilayani hapa ambae jina lake limehifadhiwa ,ambae aliuza bidhaa bila kutumia stakabadhi za efd.

Baada ya kumshawishi na kupokea hongo hiyo rashidi miraji sogoty alimwachia mfanyabiashara huyo bila kumtoza faini ya aina yoyote ,ndipo hii leo (mei 21) mshakiwa akafikishwa mbele ya mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya ya liwale, na mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana ambapo masharti ya mtu ambaye ni mdhamini wa mtuhumiwa awe mtumishi wa umma na asaini bondi ya shilingi milioni  mbili (2,000,000),mpaka  sasa mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana.

Aidha ofisi ya takukuru wilayani liwale imewataka watumishi wa umma na wananchi  kwa ujumla kuacha kabisa na vitendo vya kuomba ama kupokea rushwa kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na endapo utaonekana kutenda kosa moja wapo kati ya kuomba ama kupokea rushwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Hata hivyo wananchi kwa ujumla wametakiwa kushirikiana na ofisi ya takukuru kwa kutoa taarifa pale wanapobaini juu ya uwepo wa vitendo vya rushwa katika maeneo mbalimbali 

Post a Comment

 
Top