0
Andres Iniesta wa Barcelona
Image captionAndres Iniesta wa Barcelona
Kiungo wa kati wa Barcelona Andres Iniesta, 33, ataeleka katika klabu ya China mwisho wa msimu huu huku chupa bilioni mbili za mvinyo zikiorodheshwa katika makubaliano hayo.. (Marca - in Spanish)
Liverpool haina fursa ya kumsajili kipa wa Roma na Brazil Alisson, 25, mwisho wa msimu huu kulingana na rais wa klabu hiyo James Pallotta. (Sky Sports)
Paul Pogba na mkufunzi Jose Mourinho
Image captionPaul Pogba na mkufunzi Jose Mourinho
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kumwacha kiungo wa kati aliyenunuliwa kwa kitita cha £89m Paul Pogba, 25, kuondoka klabu hiyo pamoja na mshambuliaji Anthony Martial, 22, beki wa Uholanzi Daley Blind, 28, huku beki wa Itali Matteo Darmian akitarajiwa kuuzwa. (Mail)
Darmian, 28, anasema kuwa atafanya uamuzi kuhusu ombi la uhamisho wake kutoka klabu ya Seria A Juventus mara moja. (Express)
Manchester City itampatia meneja Pep Guardiola kitita cha £200m za uhamisho baada ya kushinda taji la ligi , huku kiungo wa kati wa Napoli na Italy Jorginho, 26, pamoja na kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk ,24, raia wa Brazil Fred wakilengwa. (Mirror)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp
Image captionMkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anatarajiwa kuanzisha tena mpango wake wa kutaka kiungo wa kati wa Napoli Piotr Zielenski. Klabu hiyo ya Itali iliishinda Liverpool kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa mika 23 2016.(Sun)
Trent Alexander-Arnold, 19, amesaini kandarasi ya muda mrefu na klabu yake ya Liverpool huku akitarajia mshahara wake kuongezeka maradufu.. (Mirror)
kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 23Haki miliki ya pichaAFP
Image captionkiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 23
Manchester United wametuma maskauti kumtazama kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 23, huku mkufunzi Jose Mourinho akitaka kuwasajili viungo wa kati wawili mwisho wa msimu.. (Mail)
Mshambuliaji wa Man United na Uingereza Marcus Rashford, 20, yuko tayari kuchelewesha kandarasi mpya na klabu hiyo baada ya kupuuzwa katika kikosi cha kwanza. (Sun)
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amekosoa hatua ya ligi ya Uingereza kuchelewesha matumizi ya mbinu ya VAR katika mechi.. (Times)
Moussa DembeleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMoussa Dembele
Tottenham iko tayari kumuuza kiungo wake wa kati Mousa Dembele, 30, na tayari wamepata wachezaji wawili wanaoweza kuchukua mahala pake.. (Mirror)
Mshambuliaji wa Atletico Madrid Fernando Torres, 34, anatarajiwa kuipuuza ligi ya kwanza ya China na badala yake kuelekea ligi ya Marekani ya MLS baada ya kutangaza kwamba ataondoka Uhispania mwisho wa msimu huu.. (Marca)
Klabu ya Boca Juniors inataka kumsajili kipa wa Juventus na Italy Gianluigi Buffon, 40Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKlabu ya Boca Juniors inataka kumsajili kipa wa Juventus na Italy Gianluigi Buffon, 40
Klabu ya Boca Juniors inataka kumsajili kipa wa Juventus na Italy Gianluigi Buffon, 40, na wanamtaka mchezaji mwenza wa zamani na mshambuliaji wa Argentina Carlos Tevez, kuwasaidia kumsajili. (Radio Continental via Mail)
Kiungo wa kati Ruben Loftus-Cheek, 22, bado hajaamua kuhusu hatma yake katika klabu ya Chelsea baada ya kuonyesha mchezo mzuri alipokuwa katika klabu ya Crystal Palace kwa mkopo . (Independent)
Rafa Benitez
Image captionKocha wa Newcastle Rafa Benitez
Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool na Fulham Danny Murphy anasema kuwa mkufunzi wa Newcastle Rafa Benitez anaweza kuwa kocha mzuri anayeweza kumrithi Arsene Wenger katika klabu ya Arsenal. (Talksport)
Mkufunzi wa Southampton Mark Hughes anasema kuwa wachezaji wake lazima wafanye kazi ya ziada iwapo wanataka kuepuka kushushwa daraja.. (Guardian)
Klabu ya Wolves inataka kutumia £20m kumsaini kwa mkopo wachezaji Benik Afobe, 25, na Willy Boly, 27 - kutoka Bournemouth na Porto mtawaliaHaki miliki ya pichaBBC SPORT
Image captionKlabu ya Wolves inataka kutumia £20m kumsaini kwa mkopo wachezaji Benik Afobe, 25, na Willy Boly, 27 - kutoka Bournemouth na Porto mtawalia
Klabu ya Wolves inataka kutumia £20m kuwasaini kwa mkopo wachezaji Benik Afobe, 25, na Willy Boly, 27 - kutoka Bournemouth na Porto mtawalia - kufuatia kupanda ngazi katika ligi ya Premia (Telegraph)
Winga wa Fulham Ryan Sessegnon, 17,anasema kuwa anataka kucheza katika ligi ya Premia licha ya klabu chungu nzima kuwasilisha maombi yao. . (Evening Standard)

Post a Comment

 
Top