Manchester City wako tayari kumuachia mlinzi wa England John Stones, mwenye umri wa miaka 23, msimu huu wa joto. (Sun)
Mshambuliaji wa Tottenham Fernando Llorente, mwenye umri wa miaka 33, ana nafasi ya kuondoka katika klabu hiyo na huedna akajiunga tena na klabu yake ya zamani Athletic Bilbao. (Mirror)
Manchester City wanaongoza jitihada za kumsajili mchezaji wa Napoli raia wa Italia mwenye umri wa miaka 26 Jorginho na mabingwa hao wa Premier League wamefanya mazungumzo ya kina na wawakilishi wa mchezaji huyo. (Mail)
Mrithi wa Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal itabidi atumei bajeti ndogo msimu huu wa joto ya kiasi ya £ milioni 50. (Telegraph)
Mkurugenzi mtendaji wa Arsenal Ivan Gazidis anaamini kuwa kapteni wa zamani wa Gunners Mikel Arteta, mwenye umri wa miaka 36, ambaye sasa ni kocha katika timu ya Manchester City, huenda akawa ndiye mrithi wa Arsene Wenger. (Sky Sports)
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Ray Parlour anaamini kuwa Meneja wa Newcastle Rafael Benitez huenda ndiye anayestahili kumrithi Arsene Wenger. (Talksport)
Arsene Wenger huenda atakuwa na nia ya kuisimamia timu ya taifa ya England siku moja anasema mwandishi wa soka ya Ufaransa Julien Laurens. (BBC Radio 5 live)
Burnley wana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa West Brom Jay Rodriguez, mwenye umri wa miaka 28, arudi Turf Moor. (Mail)
Leicester City inafikiria kumsajili beki wa kulia wa timu ya Porto raia wa Ureno Ricardo Pereira, mwenye umri wa miaka 24. (Leicester Mercury)
Meneja wa Stoke Paul Lambert na mkurugeniz anayehusika na usajili Mark Cartwright wanatarajiwa kusalia msimu ujao hata kama timu hiyo itashushwa daraja. (Stoke Sentinel)
Rais wa Roma James Pallotta anasema klabu hiyo haitaki kumuuza kipa raia wa Brazil Alisson, mwenye umri wa miaka 25, ambaye amekuwa akilenga na Liverpool. (Sky Sport Italia )
Majadiliano kuhusu kuiuza klabu ya Newcastle United kwenda kwa Amanda Staveley yatapiga hatua katika mwezi ujao iwapo wanatafuta nafasi ya kupata ufanisi. (Sky Sports)
Adam Pearson, mmiliki wa klabu ya Hull FC ya raga anaongoza mchakato wa kuinunua Sunderland. (Sun)
- Guardiola amtaka Yaya Toure aombe msamaha au asicheze tena
- Wenger athibitisha Arsenal wanamtafuta Aubameyang
Kapteni wa West Brom Chris Brunt, mwenye umri wa miaka 33, amesaini mustakabali wake kwa klabu hiyo na mchezaji huyo wa kiungo cha kati anatarajia wachezaji wengine wakuu watafuata mfano wake licha ya uwezekano wa timu hiyo kushushwa daraja katika ubingwa.(Birmingham Mail)
Huenda Liverpool ikahifadhi mamilioni ya pauni kwa mchezaji Naby Keita, mwenye umri wa miaka 23, wakati mchezaji huyo raia wa Guinea atakapojiunga na timu hiyo katika msimu ujao wa joto - ikiwa ni kutokana na matokeo duni ya RBLeipzig msimu huu. (Liverpool Echo)
Swansea wamejiunga na Celtic na Rangers katika kumsaka mchezaji wa Dundee raia wa Finland mwenye umri wa miaka 22 Glen Kamara. (Sun)
Post a Comment