0

Klabu ya soka ya Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga kwenye pambano la watani wa Jadi, lililopigwa kwenye uwanja wa taifa jioni hii na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa.


Simba ambayo imeongoza ligi kwa muda mrefu leo iliingia uwanjani ikipewa nafasi kubwa ya kushinda na pengine kwa mabao mengi zaidi, lakini bao pekee la mlinzi mkongwe Erasto Nyoni dakika 37 limeamua mchezo.

Mazingira ya mabao hilo yalianzia kwa Kevin Yondani kumchezea rafu Shomari Kapombe na kusababisha adhabu ndogo ambapo mpira huo ulipigwa na Shiza Kichuya na kutua kichwani kwa Nyoni ambaye aliutumbukiza nyavuni.

Baada ya ushindi huo Simba sasa imefikisha alama 62 kwenye mechi 26 huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi kuu msimu huu. Sasa Simba inabakiza alama 5 pekee ili iweze kuwa bingwa msimu huu.

Kwa upande mwingine kwenye mchezo wa leo Yanga walilazimika kucheza pungufu kwa takribani kipindi chote cha pili baada ya beki wa kulia Hassan Kessy kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 49 kutokana na rafu aliyomchezea Asante Kwasi.

Post a Comment

 
Top