Katika Michuano ya Cecafa challenge cup timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys hatimaye imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, (cecafa U17).Serengeti imefika hatua hiyo kufuatia kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Muyinga nchini Burundi.
Kwa ushindi huo Serengeti Boys inayofundishwa na kocha mzawa Oscar Milambo Serengeti ndiyo walioanza kufungwa bao la kwanza na baadaye kusawazisha na kisha kuongeza goli la pili.
Mabao ya Serengeti Boys katika mchezo huo yamefungwa na wachezaji Jaffar Juma dakika ya 21 na Kelvin Paul dakika ya 62 ya mchezo, sasa Serengeti Boys watakutana na mshindi wa nusu fainali nyingine baina ya Uganda na Somalia.
Post a Comment