0
Arsene Wenger
Image captionArsene Wenger
Arsenal imeanza mkakati wa kumtafuta mrithi wa mkufunzi wake anayeondoka Arsene Wenger baada ya zaidi ya miaka 22 akisimamia klabu hiyo.
The Gunners wanamtafuta mkufunzi ambaye ana sifa na maadili kama ya Wenger na anapendelea mchezo wa kusisimua mbali na kwamba anakupatia fursa ya kuonyesha ujuzi wako , kulingana na afisa mkuu mtendaji Ivan Gazidis.
Lakini ni mkufunzi gani barani Ulaya mwenye vigezo hivyo?
Waandishi James Horncastle, Raphael Honigstein na Julien Laurens wa BBC Radio 5 live wanatoa maoni yao kuhusu makocha wanaopigiwa upatu kuchukua wadfha huo.

Makocha 3 wa Itali.

Mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri, Napoli Maurizio Sarri na mkufunzi wa zamani wa Chelsea na Real Madrid Carlo AncelottiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri, Napoli Maurizio Sarri na mkufunzi wa zamani wa Chelsea na Real Madrid Carlo Ancelotti
Massimiliano Allegri, mwenye umri wa miaka 50, kwa sasa yuko katika mwaka wake wa nne na Juventus , baada ya kushinda taji la Serie A na Coppa Italia mara mbili katika kila mwaka wa kipindi cha misimu yake mitatu iliopita, huku akimaliza wa pili katika ligi ya vilabu bingwa 2015 na 2017.
Baada ya kusimamia klabu za ligi ya daraja la chini , Maurizio Sarri, 59, alichukua uongozi wa klabu ya Napoli 2015 na kuanzisha mfumo wa kushambulia ambao umeifanya klabu hiyo kuwa miongoni mwa wanaopigania taji la ligi hiyo.
Carlo Ancelotti ameshinda mataji matatu na klabu za AC Milan, Chelsea, Paris St-Germain na Bayern Munich, na pia ameshinda kombe la vilabu bingwa mara tatu , mara mbili na Milan na mara moja na Real Madrid .Raia huyo mwenye umri wa miaka 58 hajasimamia klabu yoyote tangu afutwe kazi na Bayern mnamo mwezi September.
Horncastle: "Allegri amekuwa akihusishwa na klabu kuu za Uingereza na amekuwa akisema kwamba angependelea kufanya kazi Uingereza siku moja- na kwamba klabu ya taifa hilo itamfurahisha kuiongoza.
Lakini ukitazama kilichosemwa na Gazidis sidhani kwamba Allegri ana vigezo hivyo kwasababu yeye atawaambia wakosoaji wake kwamba huwezi kuwa na ushindi kila siku mara nyengine utapata sare.
Iwapo unataka mtu anayechezesha mchezo mzuri nchini Itali , basi mkufunzi Sarri kama Gusrdiola hawezi kuwacha filosofia yake.
Anaweza kuimarisha timu ya Arsenal iliopo na hatoshinikiza kupewa fedha nyingi kuafikia hilo. Hatahivyo ana kipengee katika kandarasi yake , iwapo mtu yuko tayari kulipa Yuro 8.5m basi wanaweza kumchukua Sarri.
Napoli inajaribu kumzuia kwa kumpatia mkataba mpya ambapo atalipwa Yuro 2.5m kila mwaka .Sio Arsenal pekee bali hata klabu nyengine huenda zikawasilisha ombi zuri ambalo Napoli itashindwa kuzuia.
Honigstein: "Ancelotti sio kocha ambaye Arsenal wangetaka kwa sasa ,anaweza kuwa kocha mzuri - ambaye ni mtu atakayewasukuma wachezaji hao na kuwaambia kwamba hatutaki kuwa katika nafasi ya nne ama tano , tupiganie taji.
"Arsenal inahitaji kupata mtu ambaye hana huruma , kuondoa yale mazingira ya kukata tamaa ambayo yamekuwa yakiizonga timu hiyo kwa muda mrefu sasa. Ancelotti ataongoza mazingira kama hayo -akiwa Bayern. Alikuwa na kocha wa maungo ambaye alikuwa akivuta sigara.

The young Germans

Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel, mkufunzi wa Hoffenheim Julian Nagelsmann na kocha mkuu wa Schalke Domenico TedescoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKocha wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel, mkufunzi wa Hoffenheim Julian Nagelsmann na kocha mkuu wa Schalke Domenico Tedesco
Mkufunzi wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel, 44, amehusishwa na Arsenal lakini anaeleweka kuchukua mahala pake Unai Emery katika klabu ya Ligue 1 Paris St-Germain msimu ujao.
Julian Nagelsmann, 30, aliinusuru Hoffenheim katika hatari ya kushushwa daraja baada ya kuchukua uongozi wa timu hiyo na kumaliza katika nafasi ya nne msimu uliopita katika ligi ya Bundesliga huku wakishindwa na Liverpool katika mechi ya kufuzu katika kombe la vilabu bingwa
Domenico Tedesco, 32, yuko katika msimu wake wa kwanza na klabu ya Schalke huku klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya pili katika ligi ya Bundesliga
Honigstein: "Gazidis kama makocha vijana wa Ujerumani angejaribu naye Tuchel angependelea sana kuifunza Arsenal lakini hata yeye naye anajiunga na PSG
"Makocha Nagelsman na Tedesco wamefanya kazi nzuri wakiwa na fedha chache lakini hawauziki kwa sababu hawajafanya kazi kwa muda mrefu mbali na kuwa na uzoefu wa kushinda kombe la vilabu bingwa.
"Bayern Munich na Borussia Dortmund hivi majuzi zimejaribu kutafuta makocha kwasababu wale wanaoongoza vilabu vikuu hawapatikani .
Sioni Arsenal ikipata mkufunzi kutoka ligi ya Bundesliga -hakuna kocha ambaye ataisaidia Arsenal kuafikia malengo yake .Tuchel angekuwa kocha ambaye alifaa kumrithi Wenger lakini naye anaelekea PSG.

Luis Enrique

Luis Enrique alijiuzulu kama kocha wa Barcelona mwezi Juni uliopita baada ya kuisimamia klabu hiyo kwa miaka mitatau.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLuis Enrique alijiuzulu kama kocha wa Barcelona mwezi Juni uliopita baada ya kuisimamia klabu hiyo kwa miaka mitatau.
Kiungo wa kati wa zamani wa Real Madrid na Barcelona Luis Enrique alishinda kombe la vilabu bingwa , mataji mawili ya La Liga na lile la Copa Del Rey mara tatu katika kipindi cha miaka mitatu akisimamia klabu ya Barcelona.
Raia huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 47 ambaye pia alisimamia klabu ya Roma na Celta Vigo hajaiongoza klabu yoyote tangu aondoke Barcelona Juni iliopita.
Laurens: "Enrique alifanya kazi na mkuu wa uhusiano wa klabu ya Barcelona Raul Sanllehi. Sanllehi ana uhusiano mkubwa na Enrique, na usishangae hilo huenda likachangia Enrique kupewa kazi hiyo
Horncastle: "Enrique anatoka katika shule ya soka ya Barcelona pamoja na Guardiola - aliifunza klabu ndogo ya Barcelona kabla ya kuwa mkufunzi wa timu kubwa. Lakini ni vigumu kuona alichofanya Barcelona, alishinda mataji matatu , lakini alikuwa na Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar.
"Akiwa Roma alijaribu kubadili mafikira mbali na matokeo na kucheza mchezo mzuri, lakini waling'olewa katika kombe la Yuropa.
Aliondoka. akiwa amechoshwa na uzoefu huo licha ya kwamba alinunua wachezaji wapya . Hivyobasi ni vigumu kwa Arsenal kumuona kama muokozi.
Honigstein: "Unashindwa ni nini alichonacho Enrique- haonekani kuwa kocha mwenye ari ya kufanya kazi yake, kila mara anaonekana kuwa anayeomboleza na mtu wa siasa- Ninavyotafakari ni kwamba Gazidis na Arsenal wanataka mtu kijana na anayetaka kushinda."

Former Gunners

Mikel Arteta na Patrick VieiraHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta na Patrick Vieirawote wamechukua majukumu ya ukufunzi na klabu ya Manchester City
Mikel Arteta, 36, alicheza katika klabu ya Arsenal kwa kipindi cha miaka 5 na sasa ni naibu wa Guardiola katika Manchester City.
Patrick Vieira, 41, alishinda mataji matatu ya ligi ya Uingereza matatu ya FA katika kipindi cha miaka tisa akiwa na Arsenal na sasa ni kocha mkuu wa klabu ya New York City nchini Marekani.
Honigstein: "Arteta ametajwa mara nyingi na anaonekana kuwa kocha wa siku za usoni wa Arsenal .
Wanaweza kuishia katika hali ambayo baadhi ya majina makubwa hayapatikani ama hayana vigezo vinavyohitajika na huenda wakamchukua mtu kama Arteta ama Viera.
Mashabiki watasikitishwa sana iwapo mkufunzi wa Celtic Brendan Rodgers atapewa kazi hiyo.
Unaweza kusema kuwa wachezaji walikasirika sana wakati Wenger alipoajiriwa na Arsenal miaka 22 iliopita, lakini klabu hiyo inafaa kutoa taarifa kubwa na Arteta ama Viera anaweza kupata uungwaji mkono.
Laurens: "Arteta alionyesha mchezo mzuri alipokuwa Arsenal na vile alivyokuwa tayari kufanya kazi .
Ni mapema mno , hivyobasi hawezi kupewa kazi hiyo kwa sasa lakini sitashangaa iwapo miaka michache ijayo anaweza kuwa kocha wa Arsenal
.Shule ya Guardiola ambayo Arteta anapata mafunzo inaweza kuisaidia sana Arsenal na mashabiki wa Arsenal wangependa kuwa na mtu kama Guardiola

Post a Comment

 
Top