0
Naibu Waziri wa kilimo Dkt Mary Mwanjelwa akizungumza na wakulima wa kijiji cha legeza mwendo katika kata ya liwale B wilayani Liwale mkoani Lindi jana april 24 .
Wananchi wakiwa makini kumsikiliza Naibu wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa kwenye kijiji ch Legeza Mwendo jana april 24 wakati alipotembelea kijiji hapo kujionea hali halisi ya ugonjwa wa unyaufu Fusari ambao ugonjwa huo ushambulia mikorosho na kukauka.
 Hii ni mikorosho iliyosambuliwa na ugonjwa wa unyaufu Fusari ambao ushambulia mikorosho na kupelekea kukausha mkorosho
  Hii ni mikorosho iliyosambuliwa na ugonjwa wa unyaufu Fusari ambao ushambulia mikorosho na kupelekea kukausha mkorosho


Naibu waziri wa kilimo Dkt Mary Mwanjelwa  amewataka wakulima wilayani liwale mkoani lindi  kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa mnyauko fusari  unaoshambulia mikorosho ili kuweza kudhibiti hali hiyo isienee kwenye mikorosho mingine ambayo bado haijahathirika.

Katika kijiji cha legeza mwendo katika kata ya liwale B huku kukiwa na hali ya kukata tamaa kwa baadhi ya wakulima kufwatia mikorosho yao kuingiliwa na ugonjwa wa mnyauko fusari ambao unapelekea kukausha na kuharibu kabisa mashamba hayo .

Kufwatia janga hilo lililowakumba wakulima hawa ndipo  naibu waziri wa  kilimo Dkt mary mwanjelwa  akafunga safari na kufika katika kijiji hiki cha legeza mwendo ili kujionea hali halisi ya uharibifu wa mashamba kijijini hapo na hapa anazungumza na wakulima wa kijiji hiki huku wakulima hao wakiwa makini kusikia kile ambacho naibu waziri atawaeleza.

Dkt Mwanjwela aliwataka wakulima waliopatwa na ugonjwa huo wa fusari kwenye mashamba yao hawana budi kuchukua taadhali kwa kuikata mikorosho iliathirika na kuichoma moto ili kuweza kudhiti ugonjwa huo huku ugonjwa huko dalili zake majani kuwa njano kama kawia.


Pia naibu waziri huyo ametoa agizo kwa taasisi ya watafiti wa kituo cha Naliendele ili kuweza kupata suluhu la tatizo hilo la unyaufu wa mikorosho fusari kwa kujua ni lini tatizo hilo litakoma kama ambavyo hapa anaeleza.


Abdalah Ngojwike na Hamisi Ngonjwikwe wakulima hawa ambao wanaonyesha kukata tamaa kwa kupata mavuno kutokana na mashamba hayo  kushambuliwa vibaya na ugonjwa huo huku wakisema baadhi ya hekali mikorosho imekauka kabisa huku wakisema mpaka sasa hawajapata dawa ya kuweza kudhiti ugonjwa huo licha ya watafiki kutembelea mashamba yao.


Katika hatua nyingine Naibu Waziri DKT Mwanjelwa  ameelezea juu ya upatikanaji wa pembejeo kwa mwaka huu na kusema kuwa salfa na viuatilifu havitatolewa bure na serikali bali itatolewa kwa bei elekezi ya serikali  ambayo haitawaumiza wakulima wa zao  la  korosho.

          

Mkuu wa wilaya ya liwale Bi Sarah Chiwamba amemshukuru naibu waziri huyo kwa ujio wake na kuweza kujionea hali ya ugonjwa huo wa mnyauko fusari na kuongeza kusema kuwa zao la korosho ni tegemezi kwa wakazi wa wilayani Liwale.

    

Post a Comment

 
Top