Mkufunzi Arsene Wenger anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu hatua inayokamilisha uongozi wake miaka 22 katika klabu hiyo.
Raia huyo wa Ufaransa anaondoka mwaka mmoja kabla ya kandarasi yake ya miaka miwili kukamilika,
Arsenal iko katika nafasi ya sita katika ligi ya Uingereza na inatarajiwa kukosa katika nafasi nne bora kwa msimu wa pili mfululizo huku matumaini yao ya kushiriki katika fainali za kombe la vilabu bingwa Ualya yakitegemea iwapo watashinda kombe la ligi ya Yuropa.
Wenger mwenye umri wa miaka 68 alishinda mataji matatu ya ligi ya Uingereza na mataji manne ya kombe la FA ikiwemo makombe yote mawili mwaka 1989 na 2002
''Nashukuru kwa kupata fursa ya kuhudumia klabu hii kwa muda mrefu'', alisema Wenger.
- Ancelotti: Arsene Wenger anafaa kupongezwa
- Arsene Wenger :Taarifa ya kuondoka kwake
- Wenger awasifu mashabiki wa Arsenal
''Nimeiongoza klabu hii vizuri kwa kujitolea na maadili mema. Kwa mashabiki wote wa Arsenal , tunzeni maadili ya klabu hii''.
Arsenal imesema kuwa mrithi wake atatangazwa haraka iwezekanavyo.
Arsene Wenger anaacha sifa kubwa Afrika
Hivi maajuzi Arsene Wenger aliiambia BBC Africa kwamba t wachezaji wa kutoka Afrika wamekuwa na athari kubwa katika kazi yake katika miaka 20 iliyopita.
Ansema wachezaji wa Afrika wana arikubwa, ubunifu, wan anguvu, na wana ukakamavu ambao sio rahisi kupatikana katika soka.
Amewataja wachezaji wa Nigeria Nwako Kanu, wa Ivory Coast Kolo Toure na shujaa wa Liberia George Weah, aliyewasimamia katika klabu ya Monaco nchini Ufaransa, kama wachezaji watatu waliokuwa na athari kubwa katika kazi yake kama kocha wa timu ya soka.
Wachezaji kadhaa wamechenga ufanisi katika soka ya kulipwa chini ya ukufunzi wake katika timu ya Arsenal.
Alishinda mataji matatu ya Premier, mataji 7 ya FA na kufanikisha timu kufuza kwa ligiya mabingwa kwa miaka 20 mtawalia.
Kwa mashabiki wengu wa soka, atakumbukwa kwa jukumu lake katika kuleta mageuzi katika mchezo huo England kwa mbinu tofauti.
Mmiliki wa Arsenal na mwanahisa mkuu Stan Kroenke alielezea tangazo hilo la siku ya Ijumaa kuwa ni mojawapo ya siku ngumu zaidi katika miaka yote ya mchezo wa soka.
Aliongezea: Sababu kuu ya sisi kushirikiana na Arsenal ilikuwa kutokana na kile kilicholetwa na Arsene Wenger ndani na nje ya uwanja. Uongozi wake wa muda mrefu na ukufunzi mzuri hauwezi kamwe kuafikiwa na mtu yeyeto.
Raia huyo wa Marekani aliisifu rekodi nzuri ya Wenger akiongezea kuwa aliubadilisha mchezo wa klabu ya Arsenal na soka ya Uingereza kupitia maono yake kuhusu vile soka inavyoweza kusakatwa.
Baada ya kuajiriwa tarehe 1 mwezi Oktoba 1996, ndio meneja wa ligi ya Uingereza ambaye amehudumu kwa muda mrefu na amesimamia rekodi ya mechi 823.
Lakini mashabiki wengine wamekasirishwa na raia huyo wa Ufaransa katika misimu miwili iliopita kutokana na mchezo wao katika ligi.
Kupoteza kwa 2-1 dhidi ya Newcastle ilikuwa ya 11 katika ligi msimu huu ikiwa ni rekodi mbaya zaidi chini ya usimamizi wake, wako nyuma ya viongozi wa ligi Manchester City kwa kwa pointi 33 na pointi 33 juu ya Klabu ya Westbrom ilio chini ya jedwali ikiwa na pointi 21.
Arsenal ilimaliza nje ya timu nne bora kwa mara ya kwanza tangu Wenger awasili katika klabu hiyo na sasa wako pointi 14 nyuma ya timu iliopo katika nafasi ya nne katika jedwali la ligi Tottenham hotspurs ikiwa zimesalia mechi tano kuchezwa.
Watakabiliana na klabu ya Uhispania Atletico Madrid ambao wako katika nafasi ya pili katika ligi ya La Liga, katika nusu fainali ya kombe la Yuropa huku awamu ya kwanza ya mechi ikitarajiwa kuchezwa Alhamisi ijayo.
Matatizo yaliomkumba Wenger
Wenger alishinda mataji matatu ya ligi ya Uingereza na makombe manne ya FA katika misimu yake tisa ya akwanza akiwa mkufunzi.
Mwaka 2003-04, alikuwa mkufunzi wa kwanza tangu 1888-89 kuongoza timu ya Uingereza bila kufungwa msimu mzima .baada ya kushinda kombe la FA 2005, walisubiri miaka mingine tisa ama siku 3,283 kujipatia taji jingine . hatimaye walifanikiwa kwa kuishinda Hull City ili kuweza kushinda kombe la FA 2014kabla ya kushinda tena kombe hilo msimu uliofuatia.Kwa kuishinda Chelsea 2-1 katika uwanja wa Wembley, lakini ikamaliza pointi 18 nyuma ya kikosi cha Antonio Conte
Timu yake imeshindwa kufurukuta Ulaya tangu iliposhindwa na Barcelona katika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya 2006.
Walibanduliwa katika mondoano wa kufuza robo fainali kwa msimu wa sita mfululizo huku wakishiriki katika taji hilo 2017 mara ya mwisho na kupoteza 10-2 kwa jumla dhidi ya Bareyn Munich.
Mwaka 2006, walihamia katika uwanja wa Emirates uliogharimu £390m baada ya kuondoka Highbury
Arsenal imekuwa ikitumia fedha kidogo ikilinganishwa na wapinzani wao katika ligi ya Uingereza kuhusu usajili wa wachezaji. Lakini Wenger alivunja rekodi ya klabu hiyo mara mbili msimu huu.
Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette alijiunga na klabu hiyo katika dirisha la uhamisho kwa dau la £46.5m, huku mchezaji wake wa mwisho aliyemsajili akiwa mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang aliyegharimu £56m mwezi Januari.
Ni nani atakayemrithi?
Mkufunzi wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel tayari amehusishwa na kazi yake huku Wenger akisema kuwa mchezaji wa zamani wa Arsenal Patrick Viera ana uwezo wa kumrithi.
Tuchel anapigiwa debe na wachanganuzi kwa sasa mbele ya mkufunzi wa Ujerumani Joachim Low na mkufunzi wa zamani wa Real Madrid, AC Milan na Chelsea Carlo Ancelotti.
"Tuna malengo ya kuijenga Arsenal na kuhakikisha kuwa inashinda mataji mengi katika soka'', aliongezea Kroenke
Post a Comment