0
Mshambuliaji wa Bayern Robert Lewandowsky kuhamia Real Madrid
Image captionMshambuliaji wa Bayern Robert Lewandowsky kuhamia Real Madrid
Real Madrid imekubali mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 29, kutoka Bayern Munich msimu ujao . (Mundo Deportivo - in Spanish)
Burnley iko tayari kuongeza mshahara wa kipa Nick Pope ili kuizuia Newcastle United kumnyatia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye ameitwa katika kikosi cha Uingereza kwa mara ya kwanza kwa sasa analipwa mshahara wa £15,000 kwa wiki hukoTurf Moor. (Sun)
Ashley Young, 32 aongozewa mkataba Man united hadi 2019
Image captionAshley Young, 32 aongozewa mkataba Man united hadi 2019
Manchester United imeongeza kandarasi ya miezi 12 ya beki Ashley Young, 32, katika klabu hiyo hadi 2019. (Mail)
Takriban wachezaji 10 wa Manchester United katika kikosi cha kwanza akiwemo Michael Carrick, 36, anayestaafu na kiungo wa kati ambaye kandarasi yake imekwisha Marouane Fellaini, 30, pamoja na Zlatan Ibrahimovic, 36, huenda wakaondoka Old Trafford msimu huu (Express)
Image captionTakriban wachezaji 10 wa Manchester United katika kikosi cha kwanza akiwemo Michael Carrick, 36, anayestaafu na kiungo wa kati ambaye kandarasi yake imekwisha Marouane Fellaini, 30, pamoja na Zlatan Ibrahimovic, 36, huenda wakaondoka Old Trafford msimu huu (Express)
Takriban wachezaji 10 wa Manchester United katika kikosi cha kwanza akiwemo Michael Carrick, 36, anayestaafu na kiungo wa kati ambaye kandarasi yake imekwisha Marouane Fellaini, 30, pamoja na Zlatan Ibrahimovic, 36, huenda wakaondoka Old Trafford msimu huu (Express)
Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wanaamini beki wa kushoto Luke Shaw, 22, ananyanyaswa na meneja Jose Mourinho
Image captionBaadhi ya wachezaji wa Manchester United wanaamini beki wa kushoto Luke Shaw, 22, ananyanyaswa na meneja Jose Mourinho
Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wanaamini beki wa kushoto Luke Shaw, 22, ananyanyaswa na meneja Jose Mourinho baada ya kukosolewa pekee kufuatia ushindi wa mechi ya kombe la FA dhidi ya Brighton siku ya Jumamosi. (Telegraph)
Andres Iniesta
Image captionAndres Iniesta
Kiungo wa kati Nemanja Matic amesema kuwa viwango vya juu vya kocha Mourinho vinaweza kumfanya kuwa vigumu kufanya kazi naye lakini akaongeza kuwa anafurahia kucheza chini ya usimamizi wa raia huyo wa Ureno (Independent)
Kipa wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen, 25, amemtaka mchezaji mwenza Andres Iniesta kusalia katika klabu hiyo .Kiungo huyo wa kati anaangazia uhamisho wa kucheza nchini China.. (Sky Sports)
Thiago Silva
Image captionThiago Silva
Nahosha wa Paris Saint-Germain Thiago Silva anasema kuwa ana hakika kwamba mshambuliaji wa Brazil Neymar atasalia katika klabu hiyo, licha ya mchezaji huyo kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Real Madrid.(Canal+ via ESPN)
Neymar
Image captionNeymar
West Brom inataka mshambuliaji wa Numencia na Uhispania Guillermo, 24, kwa dau la £2m msimu ujao wakati ambapo klabu hiyo inakabiliwa na hatari ya kushushwa daraja msimu ujao. (Sun)
Aliyekuwa beki wa Arsenal na Uingereza Sol Campbell anasema kuwa amefanyiwa mahojiano ya kuwa mkufunzi wa klabu ya Grimsby Town lakini akafurushwa na klabu hiyo ya daraja la pili kwa ukosefu wa uzoefu.. (Sky Sports)

Post a Comment

 
Top