0
Paul PogbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPaul Pogba
Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amesema kwa sasa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Paul Pogba hayupo katika hali nzuri. Mshambuliaji huyo amekuwa si mtu mwenye furaha na kuonekana hapendwi na mashabiki wa soka ndani ya uwanja wao wa Old Trafford.
Pogba yupo katika kikosi cha Ufaransa kwa ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Colombia na Urusi alionekana kutopendezwa kwa kufanyiwa madadiliko na timu yake ya Manchester United katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Brighton .
Didier amesema mengi atayasikia kuhusu hilo kwa Pogba ni hali ambayo haifai, United watakuwa na mchezo mwingine wa ligi kuu dhidi ya Swansea tarehe 31 Machi.
Pogba alijiunga na United mwaka 2016 kwa ada ya pauni milioni 89 na mpaka sasa ameisaidia United kushinda Kombe la ligi na Europa League msimu uliopita.

Post a Comment

 
Top