Madaktari Hospitali ya Kenyatta wasimamishwa kazi kwa kufanya upasuaji wa kichwa kwa mgonjwa asiyestahili.
Taarifa kutoka mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo, Lily Tare, zinabainisha kuwa wagonjwa wawili waliokuwa hawajitambui na mmoja kati yao ndiye alihitaji upasuaji wa kichwa ili kuondoa damu ilionekana imeviria.
- Madaktari Tanzania wafanya upasuaji wa kihistoria
- Wanawake waandamana kuhusu madai ya ubakaji katika hospitali Kenya
Lakini pia mkurugenzi huyo ameomba radhi na kusema "tunafurahi kuwatangazia umma kwamba mgonjwa huyo sasa ametibiwa na anaenedelea vizuri"
Wafanyakazi wanaochunguzwa katika sakata hilo ni pamoja na daktari wa upusuaji wa ubongo, muuguzi, mtalaam wa dawa za usingizi.
Wakenya walivyopokea habari hizo
Wakenya wameeleza hisia zao katika mitandao ya kijamii ya Twitter.
"Jinsi mambo yanavyoharibika kwa haraka Kenya National hospital"
"Ukienda na kitambi kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta, unaweza ukute unapelekwa wadi ya wajawazito"
Hili sio sakata la kwanza kukumba hospitali hiyo, mwezi wa kwanza mwaka huu, waziri wa afya nchini Kenya Dkt Cleopha Mailu aliamrisha uchunguzi ufanyike baada ya wanawake waliojifungua kudai kwamba wanadhalilishwa kingono.
Taarifa zilizoenezwa kwenye mitandao zilidai kina mama waliojifungua wamekuwa wanashambuliwa na baadhi ya wafanyikazi wakati wakienda kwenye chumba cha watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao.
Tukio hilo liliibua maandamano na wanaharakati na wanawake walikasirishwa na usalama duni na utendaji kazi wa hospitali hiyo.
Kwa upande wa Tanzania, sakata kama hili liliwahi tokea mwaka 2007.
Tarehe 8 Novemba, madaktari wawili wa upasuaji wa ubongo katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili walimpasua kichwa Emmanuel Didas kutoa uvimbe ambao haukuwepo.
Wakati mgonjwa Emmanuel Mgaya, aliyekuwa na uvimbe huo alipasuliwa goti.
Madaktari hao walichukuliwa hatua na kufutwa kazi na mamlaka ya hospitali.
Post a Comment