0
 Afisa  Mradi  Bishara  Ahmad akitoa  maelekezo  ya  mradi kwa wadau 


Jumla  ya  shilingi  milioni 146.34  zimetolewa  na shirika  la OXFARM TANZANIA  kwa ajili ya uendesha  mradi  wa kuimarisha  usawa wa  kijinsia  na  kwezesha  kiuchumi wanawake  na  vijana kwenye  kata  za  mchinga  na  mbanja  Manispaa  ya  Lindi
Hayo  yamebainishwa  na  Afisa   Mradi Bishara   Ahmad wakati  wa  kutambulisha  mradi kwa  wadau  watao utekeleza  mradi  huo kata  za Mchinga  wilaya  Lindi  na Mbanja Manispaa  ya  Lindi
Bishara alisema mradi  unalengo  la  kujenga  na  kuwa ongezea  uwezo  wa  uelewa  wa  jamii  husani  wanawake na  vijana  kutambua   na  kuzitumia  kikamilifu  fursa  za kiuchumi na  maendeleo zilizopo   katika mazingira  yao.

Alisema  mradi  umefadhiliwa  na   shirika  la  OXFARM TANZANIA  ujumla  ya shs  milioni 146 ,342,764 utatekelezwa  katika  kata  mbili za Mbanja   Manispaa  ya Lindi  na  Mchinga
 Katibu  wa  mtandao huo  Sharifu  Maloya  alisema baada ya  kutekelezwa  mradi  huo wanatarajia  kupata  matokeo ya  kuongezeka  kwa  ushiriki  wa  wanawake  kwenye uongozi  wa  mashirika  na  taasisi , uwakilishi  kwenye ngazi   za  uongozi, na utawala  kwenye   jamii inayowazunguka na  kuwawezesha  kiuchumi  kupitia vikundi uzalisahaji  mali  vya   vijana  na  wanawake.


 Katibu  wa  mtandao  wa  Lango  mkoani  Lindi  Sharifu  Maloya  akiwakaribisha   washiriki  kwenye  kuutambulisha  Mradi  wa  Usawa  wa  kijinsia  na kuwawezesha  kiuchumi  wanawake  na vijana 
 Wadau  wakifutilia  maelezo  ya   mratibu  wa mradi 
Afisa Mradi   Lango  Bishara akiwasilisha  maada  kwa  washiriki wakati  wa  kutambulisha  mradi  wa  kuimarisha  usawa  wa  kijinsia  na  kuwawezesha  kiuchumi  wanawake  na  vijana katika  kata  za  Mbanja  na  mchinga Lindi

Post a Comment

 
Top