
Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka bora ya mwaka 2017 nchini Ureno.
Rolnado alitangazwa Kupitia hafla iliyofanyika mjini Lisbon, baada ya kuwashinda wachezaji Bernardo Silva wa Manchester city na golikipa wa klabu ya Sporting Lisbon Rui Patricio.
Ameshinda tuzo hiyo baada ya kuisaidia Real kushinda mataji yote ya La Liga na ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo mwaka huu 2017.
Naye Kocha wa klabu ya Monaco Leonardo Jardim ameshinda tuzo ya Kocha Bora, baada ya kuiongoza timu hiyo ya Ufaransa kushinda taji la Ligue 1 na kufika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, wakati kocha wa Manchester United, Jose Mourinho yeye ameshinda tuzo ya Vasco da Gama kwa kulitangaza vyema soka la Ureno kimataifa.
Post a Comment