0

MSICHANA mwenye umri wa miaka 25, Anastazia Elias, mkazi wa Kata ya Kipindu wilayani Nkasi mkoani Rukwa, amenusurika kifo baada ya kuokolewa na polisi akituhumiwa kumuua mtoto wake baada ya kujifungua.

Majirani wa msichana huyo aliyetambuliwa kama Mama Bara, walilieleza gazeti hili kuwa mama huyo ana mtoto wa mwaka mmoja, na alimuachisha kunyonya, na kwamba alikuwa akiishi na bibi yake.

Wananchi wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mawe walianza kumshambulia mwanamke huyo wakimtuhumu kumuua mwanawe wa kiume baada ya kujifungua ambapo alimviringisha na vipande vya khanga na kuweka kwenye kikapu alichokifi cha chini ya uvungu wa kitanda chake. Kamanda wa Polisi wa Mkoa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi saa nane mchana katika Kijiji cha Kipundu kilichopo mjini Namanyere wilayani Nkasi.

Kamanda Kyando alisema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi wilayani Nkasi kwamba atafi kishwa mahakamani baada ya upelelezi wa awali wa tukio hilo kukamilika. Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya wanawake kwa masharti ya kutoandikwa majina yao, walidai mtoto huyo alizikwa juzi usiku katika kaburi lililochimbwa ndani ya nyumba ambayo mama yake mzazi anaishi na bibi yake.

Akisimulia mkasa huo, Diwani wa Kata ya Kipundu, John Kapandila alisema mchana wa siku ya tukio, watoto wadogo walimuona mwanamke huyo akiwa amebeba kitu kwenye mfuko wa plastiki na kwenda chooni alipotoka hakurudi nao. “Watoto hao walikimbia na kuwataarifu wazazi wao kuwa Mama Baraka amejifungua mtoto, lakini amemtupa chooni....

Wazazi hao walienda mbio nyumbani kwa mzazi huyo kwa mshangao wao walimkuta akipepeta mahindi nje ya nyumba alimokuwa akiishi. “Walimpa hongera huku wakitaka kumuona mtoto, lakini aliwakatalia akidai kuwa hajajifungua na kwamba hakuwa na mimba,” alidai diwani huyo. Kwa mujibu wa diwani, wananchi hao walimhoji huku wakitishia kumpiga ndipo alipokubali kuwa amejifungua muda mchache uliopita.

“Wananchi hao walienda chooni na wakafanikiwa kutoa mfuko wa plastiki na kubaini kuwa kilichokuwemo humo ilikuwa ni kondo ‘placenta ‘ na sio mtoto kama walivyoelezwa. Ndipo alipowapeleka chumbani kwake na kuwaonesha mtoto alipo ambapo alikuwa amefungwa na vipande vya khanga na kuwekwa kwenye kikapu, bila shaka alikuwa akisubiri muda ufi ke akamtupe,” alieleza diwani. Inadaiwa wananchi hao walipandwa na hasira wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumshambulia ndipo askari polisi walipofi ka eneo hilo la tukio na kumwokoa.

IMEANDIKWA NA PETI SIYAME- HABARILEO NKASI

Post a Comment

 
Top