0
Mshambuliaji wa City Aguero akihusika katika mzozo na mmoja wa mashabiki baada ya mechi hiyoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa City Aguero akihusika katika mzozo na mmoja wa mashabiki baada ya mechi hiyo
Wigan Athletic ilisitisha matumaini ya ManCity ya kupata mataji mengi baada ya kuwashangaza katika mechi ya raundi ya tano ya kombe la FA.
Klabu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza nchini Uingereza ilistahimili presha ya mara kwa mara kutoka kwa viongozi hao wa ligi ya EPL na kutumia fursa ya kadi nyekundu aliyopewa Fabian Delph wakati Will Grigg alipofunga katika dakika 11 kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo.
Shambulizi hilo la kimo cha nyoka lilizua vioja katika uwanja wa DW stadium huku kiungo wa kati wa City Fernandinho akikosa nafasi ya wazi muda mfupi baada ya Delph kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo Max Power.
Kisa hicho kiliwafanya makocha wote wa pande zote mbili kurushiana maneno wakati wa muda wa mapumziko.
Na kulikuwa na vioja zaidi baada ya mechi hiyo kukamilika huku mshambuliaji Sergio Aguero akihusishwa na mzozo na mmoja wa mashabiki waliovamia uwanja huo.
Kulikuwa na vioja baada ya mchezaji wa City Fabian Delph kupewa kadi nyekundi kwa kumchezea visivyo Max Power.
Image captionKulikuwa na vioja baada ya mchezaji wa City Fabian Delph kupewa kadi nyekundi kwa kumchezea visivyo Max Power.
City waliwashambulia wenyeji wao baada ya bao hilo la Grigg ambalo lilikuwa shambulio kutoka maguu 20 huku kichwa cha Danilo kikidakwa na kipa Christian Walton katika dakika za lala salama.
Na mpira ulipokamilika kulikuwa na shangwe na nderemo ndani ya uwanja kutoka kwa mashabiki wa nyumbani.
Kwa upande mwengine mashabiki wa City walikuwa wamekasirika na vitu vilirushwa ndani ya uwanja baada ya wachezaji kuondoka.
Mchezaji wa Wigan aliyefunga bao la pekee GriggHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMchezaji wa Wigan aliyefunga bao la pekee Grigg
Lakini hilo halikuaribu usiku wa Wigan walioishinda City katika kombe hilo kwa mara ya tatu ndani ya misimu sita.

Post a Comment

 
Top