0
Wahitimu 415 wa mafunzo ya usalama barabarani wakiwa kwenye ukumbi wa tengeneza wakati mkuu wa wilaya ya Liwale Bi Sarah Chiwamba akifunga mafunzo ya usalama barabarani leo Februari 2018.(Picha na Liwale Blog)
   Mkuu wa wilaya ya Liwale Bi Sarah Chiwamba ambaye ni mgeni rasmi 

Madereva wanaotumia vyombo vya moto wilayani Liwale mkoani Lindi wametakiwa kuwa makini katika kutumia barabara pamoja na kutii sheria za usalama barabarani.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Bi  Sarah Chiwamba wakati wa kufunga mafunzo ya sheria za usalama wa barabarani ambapo yameendeshwa kwa takrabani ya wiki mzima kwenye kata mbalimbali kama kata ya Kichonda,Mbaya,Mihumo,Liwale B,na kufunga leo Februari 24 katika ukumbi wa Tengeneza ,ambapo yamejumuisha wahitimu 415 miongoni mwao wanawake wawili tu.

Pia mkuu wa wilaya alisema kuwa kama sheria zitazingatiwa ipasavyo na kutumia sheria za usalama barabarani vizuri kuna uwezekano mkubwa wa wimbi la ajali litapungua kwa kiasi kikubwahuku akiwataka wahitimu hao kuwa mabalozi kwa waliokosa elimu wanatakiwa kuwashawishi wasiopata elimu waweze kujitokeza kupata elimu ya usalama barabarani.

Mafunzo hayo yametolewa na Anti poverty And Enviromentel Care ( APEC) yakiwa na malengo ya kupunguza ajali za barabarani na kuwapa fursa mbalimbali vijana.

Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo cha Anti poverty And Enviromentel Care ( APEC) Respicius Timanywa alisema kuwa lengo ni kuwafundisha vijana waendesha vyombo vya moto lengo ni kuwapa fursa vijana na kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano ili kuhakikisha sekta ya viwanda inakuwa kwa kasi.

Hata hivyo wahimu wa mafunzi hayo ya usalama barabarani Kindamba Manyai alisema kuwa amenufaika kwa kuzifahamu alama za usalama barabarani anaamini kuwa kutakuwa na punguzo la ajali za barabarani.

Nae Bi Zubeda Nyimwe alisema kuwa mafunzo ameyapokea vizuri huku akiwataka wanaume wawaimize wanawake kujitokeza kwa wingi kwenye mafunzo ya usalama wa barabarani aliongeza kusema kuwa wanawake wanawajibu wa kutumia vyombo vya moto pia.


 Wahitimu wa mafunzo ya usalama wa barabarani akiwa kwenye maandano
  Wahitimu wa mafunzo ya usalama wa barabarani akiwa kwenye maandano


  Wahitimu wa mafunzo ya usalama wa barabarani akiwa kwenye maandano



 Msoma risala ndugu Zuberi Libena akisoma mbele ya mgeni rasmi  kwa niaba ya wahitimu






 Mkurugenzi wa chuo cha Anti poverty And Enviromentel Care ( APEC) Respicius Timanywa



 Viongozi mbalimbali waliweza kukabidhiwa zawadi kutoka kwa wahitimu ilikuwa kuonesha upendo na ushirikiano 




Post a Comment

 
Top