0
Alexis Sanchez akitia saini mkataba wa kuhamia Manchester United kutoka Arsenal
Image captionAlexis Sanchez akitia saini mkataba wa kuhamia Manchester United kutoka Arsenal
Alexis Sanchez ametoka katika klabu ''nzuri'' na kuhamia klabu ''kubwa'' baada ya mchezaji huyo kujiunga na Manchester United kutoka Arsenal kulingana na mkufunzi wake mpya Jose Mourinho.
Mchezaji huyo wa Chile alielekea Old Traford kwa kubadilishana na kiungo wa kati raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan.
Mourinho amesema kuwa ulikuwa mkataba mzuri kwa kila mmoja na kuthibitisha kuwa Sanchez atajumuishwa katika kikosi cha United cha kombe la FA raundi ya nne dhidi ya Yeovil siku ya Ijumaa.
Mechi hiyo itaonyeshwa moja kwa moja katika kituo cha habari cha BBC One na mtandao wa BBC Sport.
Sanchez mwenye umri wa miaka 29 ambaye karibu ajiunge na Manchester City mwishoni mwa msimu uliopita ametia saini kandarasi ya miaka minne na nusu yenye thamani ya £14m kwa mwaka baada ya kulipa kodi.
Aliifungia Arsenal mabao 80 baada ya kuhamia katika klabu hiyo kutoka Barcelona mwezi Julai 2014 ,na msimu uliopita alikuwa na mabao 30 katika mashindano yote.
''Tuna mmoja ya washambuliaji wazuri zaidi duniani," alisema Mourinho. ''Ni muhimu sana kwa sababu tunahitaji wachezaji wazuri zaidi''.
''Kwa sababu amekuwa Uingereza kwa muda mrefu, nadhani kila mtu anajua kiwango cha mchezo wake akiichezea Arsenal. Najaribu kutozungumza kuhusu alichofanya kabla ya kuelekea Uhispania na Italia lakini katika ligi ya England ameonyesha kiwango cha juu cha mchezo''.
Mkufunzi wa Man United Jose Mourinho anasema kuwa Sanchez alihamia timu kubwa
Image captionMkufunzi wa Man United Jose Mourinho anasema kuwa Sanchez alihamia timu kubwa
Mchezaji wa zamani wa Dortmund Mkhitaryan mwenye umri wa miaka 29 alifunga mabao 13 katika mechi 63 za United ikiwemo moja ambalo alifunga katika siku ya fainali ya kombe la Yuropa dhidi ya Ajax.
Lakini alishiriki mechi 10 pekee za ligi ya Uingereza msimu huu na inaaminika kulikuwa na uvunjikaji wa imani kati yake na mkufunzi wa United Jose Mourinho.
Mourinho alisema: "Nadhani ulikuwa mkataba mzuri na mkataba ulio mzuri ni mzuri iwapo umependelewa na kila mtu.
''United na Arsenal ziliweka makubaliano mazuri, nilipoteza mchezaji mzuri, BwWenger naye akapoteza mchezaji mzuri, Alexis Sanchez alitoka katika klabu nzuri na kuhamia katika klabu kubwa naye Mkhitaryan akahamia katika klabu nzuri kwa hivyo ulikuwa mkataba mzuri kwa kila mtu''.
''Naamini kwamba Mkhitaryan huenda akawa mzuri zaidi ya alivyokuwa nasi''.
"Huku akiwa na mwaka mmoja na nusu Uingereza, amezoea, nadhani ni mkataba mzuri kwa kila mtu, hiyo ndio sababu namfurahia Mkhitaryan.
"Je anaweza kucheza vyema zaidi nasi, je nitavuna kutoka kwa kipaji chake? Pengine. Je pengine ataonyesha mchezo mzuri zaidi akiwa nasi ? Pengine, lakini sidhani kuna majuto, yuko katika historia yetu."

Post a Comment

 
Top