0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua kuelekea Baharini katika maeneo ya Ilala Bungoni na Temeke kwa Aziz Ally Jijini Dar es Salaam leo. Mifereji hiyo inajengwa ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo lengo ni kunusuru hali ya mafuriko katika maeneo hayo. Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando..
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa mafundi wa wanaojenga mfereji wa maji taka eneo la Ilala Bungoni alipotembelea mradi huo leo Jijini Dar es Salaam


Sehemu ya mfereji unaojengwa katika eneo la Ilala Bungoni kwa ajili ya kupeleka maji hadi katika bonde la mto msimbazi ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo mafuriko.
Sehemu ya mfereji unaojengwa katika eneo la Temeke kwa Aziz Ally kwa ajili ya kusafirisha maji ya ikiwa ni njia ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo mafuriko.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiulizia jambo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa mfereji wa maji katika eneo la Ilala Bungoni leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiulizia jambo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa mfereji wa maji kuelekea baharini katika eneo la Temeke kwa Aziz Ally leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba.


Picha na: Frank Shija – MAELEZO


………………..


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wanaoishi kwenye mpaka kati ya Buguruni Mivinjeni na Sharifu Shamba pamoja na Mtoni kwa Azizi Ali kuwa watunzaji wazuri wa mitaro ya maji kwani ni mali yao wenyewe na si ya serikali.

Makamu wa Rais aliyasema hayo wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kuta za bahari na mitaro ya maji jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais aliwaeleza wananchi hao kuwa mabadiliko ya tabia nchi yameathiri shughuli za kiuchumi , kijamii na kimazingira.

Makamu wa Rais Makamu wa Rais alisema kila mmoja anapaswa kujishughulisha katika suala la kusafisha na kuhifadhi mazingira .“ubaya wa mazingira ukiyaharibu yanakuadhibu” alisisitiza Makamu wa Rais.Mtaro wa Buguruni Mivinjeni una urefu wa mita 475 na ule wa kwa Azizi Ali una urefu wa mita 550.

Makamu wa Rais alisema nchi inapozungumzia uchumi wa viwanda ni mazingira “tukiharibu mazingira hamna uchumi wa viwanda” hata viwanda vitakavyojengwa vinahitaji kutunza mazingira, visafishe maji yake kabla ya kutiririsha.

Makamu wa Rais alitoa rai kwa yeyote atakayebainika kuharibu miundo mbinu wanachukuliwa hatua za haraka.Makamu wa Rais alimalizia kwa kusema kuwa Usalama wa Nchi, Amani, afya, mazingira bora hayana chama hivyo ni jukumu la kila mmoja kuwajibika ili maendeleo yaweze kupatikana.

Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema kuongezeka kwa watu katika jiji la Dar es Salaam na mabadiliko ya tabia nchi kutaendelea kutoa changamoto za miundo mbinu hivyo Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kujenga miundo mbinu itakayowezesha wananchi kuendelea na shughuli zao kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo.

Post a Comment

 
Top