0
Mbwana Samatta
Image captionMbwana Samatta
Mchezaji wa soka kutoka Tanzania Mbwana Samatta amechaguliwa kuwa kijana mwenye ushawishi mkubwa nchini Tanzania kulingana na kura ya maoni iliofanywa na chombo cha habari cha Avance media.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaichezea klabu ya Genk na timu ya taifa ya soka nchini humo taifa Stars.
Nahodha huyo wa Tanzania alishinda tuzo ya mchezaji bora wa shirikisho la soka barani Afrika Caf miongoni mwa wachezaji wanaosakata kandanda barani Afrika 2016 baada ya kuisaidia timu yake ya TP Mazembe kushinda kombe la ligi ya Afrika.
Wema Sepetu ni miongoni mwa vijana walio na ushawishi mkubwa nchini Tanzania
Image captionWema Sepetu ni miongoni mwa vijana walio na ushawishi mkubwa nchini Tanzania
Naye mtangazaji wa habari wa BBC Swahili Salim Kikeke alikuwa wa saba katika kura hiyo akimshinda msanii wa bongo fleva Diamond Platinumz.
Samatta: Kupigania tuzo CAF ni heshima kwa Tanzania
Matokeo ya kura hiyo nchini Ghana na Nigeria yalitolewa mapema mwaka huu.
Nyota wa muziki wa bongo fleva Diamond Platinumz
Image captionNyota wa muziki wa bongo fleva Diamond Platinumz
Mchezaji Victor Moses alichaguliwa kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa huku wakili wa rais wa Ghana Kow Essuman akichaguliwa mtu mwenye ushawishi mkubwa nchini humo.
Tazama orodha kamili ya vijana walio na ushawishi mkubwa Tanzania:
Orodha ya vijana walio na ushawishi mkubwa nchini TanzaniaHaki miliki ya pichaAVANCE MEDIA
Image captionOrodha ya vijana walio na ushawishi mkubwa nchini Tanzania


Post a Comment

 
Top