Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ''alitukosea heshima'' kwa kuzungumza hadharani kuhusu mchezaji Pierre-Emerick Aubameyang, amesema mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Borussia Dortmund Michael Zorc.
Arsenal ina hamu ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Gabon kwa dau la £60m.
- Aubameyang: Mwafrika anayevuma Ujerumani
- Aubameyang aachwa nje katika kikosi cha Dortmund
- AFOTY: Wasifu wa Pierre-Emerick Aubameyang
Siku ya Alhamisi , Wenger alisema kuwa Aubameyang atafaa sana Arsenal , matamshi ambayo hayakuifurahisha klabu ya Dortmund.
''Tunahisi kwamba ni kukosa heshima kwa Wenger kuzungumzia kuhusu wachezaji wa klabu nyengine'', alisema Zorc.
''Hatujawasiliana na Arsenal''.
''Kwa sasa Arsene Wenger ana maswala mengi yanayompa changamoto ikiwemo mchezo wa wachezaji wake''.
Aubameyang ameadhibiwa mara mbili kwa utovu wa nidhamu msimu huu.
Alikosa mechi ya Jumapili ya sare ya 0-0 dhidi ya Wolfsburg baada ya kukosa kuhudhuria mkutano wa timu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ni mfungaji wa mabao mengi katika timu hiyo msimu huu baada ya kufunga mabao 13 katika mechi 15.
Dortmund ni ya nne katika ligi ya Bundesliga, wakiwa na alama 15 nyuma ya viongozi wa ligi Bayern Munich
Post a Comment