0
Klabu ya Yanga inatarajiwa kushuka dimbani leo jumapili ya Desemba 24.2017 kuwakabili klabu ya Reha Fc inayoshiriki ligi daraja la pili katika pambano litakalopigwa kunako uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Mchezo huo ni mwendelezo wa michuano ya kombe la shirikisho Tanzania (ASFC) Na untarajiwa kutimua vumbi kuanzia majira ya saa 16:00 jioni ya leo.
Yanga watashuka dimbani bila kocha wao Mzambia, George Lwandamina kutokana na msiba alioupata wa kuondokewa na mwanaye.
Vilevile yanga inaweza kuwakosa nyota wake watatu ambao ni walinda mlango wasaidizi, Benno Kakolanya na Ramadhani Kabwili kwa kile kinachoelezwa kuwa ni maradhi yaliyowapata.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa meneja wa klabu hiyo,Hafidh Saleh zinaeleza kuwa Kakolanya anaumwa Malaria huku Kabwili akisumbuliwa na maradhi ya tumbo.
Hata hivyo amemtaja golikipa wa timu ya Yanga B, Mussa Mbise kuwa ndie atakaye kalia benchi akiwa kama msaidizi wa Youthe Rostand.
Aidha klabu hiyo inaweza kumkosa mlinzi wake wa kati, Kelvni Yondani ambae anasumbuliwa na kifundo cha mguu majeraha aliyoyapata akiwa nchini Kenya katika michuano ya CECAFA akiwa na timu ya taifa ya Kilimanjaro Stars.
Ili kuepuka yasiwakute kama yaliyotokea kwa Simba, Yanga wanatakiwa kushinda mchezo huo ili kusonga mbele katika michuano hiyo ambayo kwa sasa ipo katika hatua ya mtoano

Post a Comment

 
Top