0
Vurugu zimeendelea huko ukanda wa gaza
Image captionVurugu zimeendelea huko ukanda wa gaza
Vurugu zimeendelea huko ukanda wa gaza na ukingo wa magharibi ambapo zaidi ya wapalestina thelathini wamejeruhiwa katika makabiliano na polisi wa Israel
Hii ni kufuatia Rais Donald Trump kutangaza kuutambua mji wa Yerusalemu kuwa mji mkuu wa Israel.
Wakati huo huo Marekani imeionya Palestina dhidi ya maamuzi yake kutotaka kukutana na makamu wa rais marekani ,Mike Pence katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika mapema mwezi huu.
Waandamanaji wamechoma matairi na kurusha mawe huku maafisa usalama wa Israel wakifyatulia wandamaanaji hao hewa ya kutoa machozi na risasi za mpira.
Israel wakifyatulia wandamaanaji hao hewa ya kutoa machozi na risasi za mpira
Image captionIsrael wakifyatulia wandamaanaji hao hewa ya kutoa machozi na risasi za mpira
Huko Gaza kundi la kiislamu la Hamas limeitisha intifada au mapambano. Omary Shakir mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch katika eneo la Isreal na Palestina yupo mjini Ramala.
Ameiambia BBC kuwepo baada ya Israel katika eneo hilo kwa miongo kadhaa sasa wapelestina wengi wamekuwa na hasira na tangazo la Rais Trump.
Kwa upande wake Naibu waziri anayehusika na masuala ya Diplomasia wa Israel Michael Oren ameimbia BBC kuwa tangazo la Rais Trump limeleifanya iwe siku ya furaha kwa kwa taifa la Israel ameseema mamlaka ya Israel ilitarajia vurugu kutoka kwa wapalestina.
Vurugu zaidi zinatarajia kuendelea hii leo huku kikao cha dharara baraza la usalama la umoja wa mataifa kinatarajiwa kutoa maamuzi mazito kuhusu tamko hilo la rais Donald Trump.

Post a Comment

 
Top