Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania bara Elias Maguri amesema kwasasa ni mchezaji huru mara baada ya mkataba wake kuwa umeisha katika klabu aliyokuwepo huko Uarabuni huku akiweka wazi kuwa tayari Vilabu kadhaa tayari vimeshaanza kumuwinda.
Yanga ni moja kati ya Klabu inayotajwa sana kuwa ipo katika mchakato wa kumnasa Maguri lakini yeye Mwenyewe alipoulizwa kuhusu Yanga alisema kuwa hiki ni kipindi cha usajili kwahiyo watu wategemee jambo lolote na Kuhusu Pololwane kumwitaji pia alifunguka haya.
” Hiki ni kipindi cha usajili kwahiyo mambo mengi yanaweza kutokea, siyo Yanga tu kuna vilabu vingi, Kuhusu kuhitajika Polokwane City ya Afrika kusini bado tupo kwenye mazungumzo nafikiri kama mambo yakikamilika nitaweka kila kitu wazi. “
Post a Comment