m
mkutano Mkuu wa 54 wa chama tawala nchini Afrika kusini cha African National Congress (ANC) unafanyika huku agenda kubwa ikiwa ni nani atarithi uongozi wa chama cha ANC kutoka kwa Rais Jacob Zuma.
Rais Zuma ambaye aliingia madarakani akimrithi Thabo Mbeki, amekuwa akiandamwa na kashfa za ufisadi kwa muda mwingi wa uongozi wake, kumekuwa na jitihada za kumvua madaraka na kumburuza mahakamani ambazo zimekuwa zikigonga mwamba.
Kinyanganyiro hiki cha uongozi kinakutanisha watu sita ingawa ni wawili wenye kupewa nafasi kubwa.
Wa kwanza ni mke wa zamani wa Rais Zuma, Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye pia amewahi kuwa kiongozi wa AU, wa pili ni Makamu wa rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa ambaye ni mmoja wa matajiri wakubwa Nchini Africa ya kusini.
Pamoja na kujikwamua kutoka kwenye ubaguzi, wengi wa wananchi wa Afrika ya kusini bado wanaishi kwenye maisha duni huku Nchi hiyo ikiwa ni moja ya Nchi zenye utajiri mkubwa wa maliasili na uchumi mkubwa barani Afrika.
Post a Comment