Mvua iliyo ambatana na upepo mkali umeacha Familia 100 hazina makazi kufuatia nyumba zao kubomoka na kuezuliwa usiku wa kuamkia leo disemba 16 ambapo nyumba 60 na vyumba vitano vya madarasa ya shule ya msingi Chandamali kata ya Bombambili manispaa ya Songea vimeezuliwa.
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Songea chini ya mwenyekiti wake mkuu wa wilaya Pololeti Mgema wamewatembelea wananchi waliokumbwa na kadhia hiyo kwa lengo la kutoa pole kwa wahanga.
Serikali imewataka wananchi kuzingatia kanuni bora za ujenzi kwani nyumba nyingi zilizoezuka zimejengwa bila kuzingatia kanuni za ujenzi, aidha serikali itaelekeza nguvu zake kukarabati vyumba vitano vya shule ya msingi Chandamali hivyo wananchi waanze kukarabati nyumba zao bila kusubiri msaada.
Wakati huo miundo mbinu ya Tanesco nguzo zimedondoka na nyaya za umeme kusambaa hovyo, aidha huko Matimila halmashauri ya wilaya ya Songea nyuma 15 zimeezuka na jengo la utawala la sekondari ya Matimila gharama za hasara iliyotokana na maafa hayo bado haijafahamika serikali inaendelea kukusanya taarifa sahihi
Post a Comment