Beki wa Kilimanjaro Stars, Gadiel Michael, akimiliki mpira wakati wa mchezo wa kwanza wa timu hiyo dhidi ya Libya katika michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Machakos nchini Kenya. Katikamchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 0-0.
Erasto Nyoni akichanja mbuga katikati ya wachezaji wa Libya.
Mbaraka Yusuf akimiliki mpira mbele ya beki wa Libya...
Elias Maguli (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Libya.
TIMU ya Kilimanjaro Stars ya Tanzania, leo imetupa karata yake ya kwanza dhidi ya Libya katika michuano ya Cecafa Challenge Cup iliyoanza leo jijini Nairobi nchini Kenya.
Katika mchezo huo uliokuwa wa kushambuliana kwa zamu na spidi kali kwa timu zote zilionekana kutulia huku zikishambuliana kwa zamu lakini hadi dakika 90 zikimalizika katika Uwanja wa Machakozi timu hizo zimetoka sare ya 0-0.
Katika mchezo wa fungua dimba katika mashindano hayo kati ya wenyeji Kenya na Rwanda, Wenyeji Kenya walishinda mabao 2-0.
Post a Comment