Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo
Wananchi wakifurahia baada ya uzinduzi huo
Muonekano wa zahanati hiyo ya Ilindiwe
Mwenyekiti wa Kijiji akitoa taarifa fupi ya Ujenzi huo
Mganga Mfawidhi Dk Leonard akizungumza na wananchi
Afisa mtendaji kata ya Mang'oto Mengi Chalamila akizungumza kwenye uzinduzi huo
Mgeni Rasmi akitoa hotuba yake
Mganga mfawidhi akimweleza jambo Mgeni Rasmi ndani ya zahanati hiyo
Muonekano wa Mbele wa zahanati hiyo
Hatimaye zahanati ya kijiji cha Ilindiwe wilayani Makete mkoani Njombe iliyokuwa haijaanza kufanya kazi kwa miaka 5 baada ya kujengwa, imezinduliwa hii leo tayari kwa kuanza kuhudumia wananchi wa kijiji hicho
Zahanati hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa imejengwa na wananchi pamoja na mchango wa serikali mpaka inazinduliwa imegharimu shilingi milioni 52.3
Akisoma taarifa fupi ya zahanati hiyo mwenyekiti wa Kijiji cha Ilindiwe Bw. Yosofati Idawa amesema wananchi waliona umuhimu wa kuwa na zahanati hivyo walijitoa usiku na mchana kuhakikisha inakamilika, huku akizungumzia baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo kusuasua kutekelezwa kwa ahadi walizoahidiwa wakati wakiendelea na ujenzi wa zahanati hiyo
Mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Bw. Leonard Mlwilo amewaomba wananchi hao kujiunga mafuko wa afya ya jamii CHF ambao utasaidia kuimarisha zahanati hiyo hasa kwa upande wa dawa
Diwani wa kata ya Mang'oto ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa zahanati hiyo amewashukuru na kuwapongeza wananchi hao kwa michango yao ya hali na mali iliyofanikisha kukamilika kwa zahanati hiyo
Amesema changamoto ya rasilimali mbao kama meza na viti wananchi waendelee kujitolea kuhakikisha vinakuwepo kwa kuwa rasilimali hiyo inapatikana kijijini hapo, huku pia akiwasisitiza kuweka utaratibu wa kukusanya mchango wa CHF ikibidi uanze mapema ili manufaa yaende sanjari na kuanza kutumika kwa zahanati hiyo
Kuanza kutumika kwa zahanati hiyo kutawaondolea kero wananchi wa kijiji hicho ambao walikuwa wakisafiri umbali mrefu hadi kijiji cha Mang'oto kufuata huduma za kiafya Jambo lililofurahiwa na wananchi hao










Post a Comment