0
Wamiliki wa klabu ya Leicester City nchini Uingereza Vichai Srivaddhanaprabha na mwanawe AiyawattHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWamiliki wa klabu ya Leicester City nchini Uingereza Vichai Srivaddhanaprabha na mwanawe Aiyawatt
Wamiliki wa klabu ya Leicester City nchini Uingereza wamedaiwa kushtakiwa kwa umiliki wa £323m zinazodaiwa na serikali ya Thai.
Mahakama ya jinai nchini Bangkok ilikubali kesi dhidi King Power International siku ya Jumatatu , kulingana na shirika la habari la Reuters.
Kesi hiyo pia itawasilishwa dhidi ya maafisa wanaomiliki uwanja wa ndege wa taifa wa Thailand(AOT) Reuters imesema.
BBC imewasiliana na klabu hiyo ya Leicester City FC , King Power na AOT kwa maoni yao.
Makahakama hiyo inailaumu King Power kwa kukosa kuilipa serikali ya Thai bilioni 14 baht (£323m) kutoka kwa operesheni ya kufanya biashara bila kulipa ushuru tangu mwaka 2006.
Kwa kusikilizwa kwa kesi hiyo siku ya Jumatatu , mahakama hiyo ya jinai huko Bangkok iliikubali kesi hiyo na kusema iko tayari kusikiliza upande wa ushahidi mwezi Februari mwaka ujao.
Hatua hiyo dhidi ya kampuni ya King Power, inayomilikiwa na Vichai Srivaddhanaprabha na familia yake iliwasilishwa mwezi Julai.

Post a Comment

 
Top