Wajasirimali nchini wameiomba serikali kupunguza urasmu wa upatikanaji wa alama ya ubora wa bidhaa wanazozitengeneza ili waweze kuingia kwenye ushindani wa soko la ndani na nje.
Ombi hilo limetolewa na wajasiriamali wa walioshiriki maonesho ya sido kanda ya kusini , mashariki yanayofanyika uwanja wa Ilulu mkoani Lindi
Isa Mkomozi Alisema kuwa wajasirimali wamekuwa na kero ya muda mrefu ambayo haina utekelezaji kwani wajasirimali wengi wanashindwa kupata alama ya ubora wa bidhaa kutoka TBS pamoja na huduma hiyo utolewa bure
Mkomozi Alisema kitendo cha TBS kutokuwa na ofisi wilayani kuna sababisha wajasiriamali kupata usumbufu na kukata tama hali ambayo inapelekea bidhaa nyingi za wafanyabiashara wadogo kukosa alama ya TBS.
Wajasirimali tunachangamoto nyingi mfano TBS hawapo kila mkoa hii ina sababishia kupata usumbufu na kukata tama kwani gharama bado ni kubwa ndiyo maana maonesho haya bidhaa nyingi hazina alama ya ubora na hata mwakani pia utaona hivyo hivyo Alisema
Mkurugenzi wa sido Prof Eng Sylvester Mpanduji amewataka wananchi mkoani Lindi kutumia fursa waliyoipata ya maonyesho ya wajasiriamali wadogo na wa kati Kanda ya kusini, mashariki kwa kujitangaza kibiashara na kujifunza kutoka kwa wenzao ndani na nje ya nchi.
Mpanduji aliongeza kuwa hadi hivi sasa sido imetoa mikopo kwa vikundi vya wajasirimali 4034 nchini wenye thamani ya shilingi billion 1.5 ambayo marejesho yake yamekuwa mazuri
Post a Comment