WAJASILIAMALI wa mikoa ya kanda ya kusini mashariki wenye viwanda vidogo wamehimizwa kuacha kuuza bidhaa wakiwa ndani ya nyumba zao badala yake wajitokeze na waanze kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango vitakavyowasaidia kuweza kupeleka bidhaa zao kwenye soko la kimataifa.
Wito huo ulitolewa jana mkoani Lindi na mkuu wa mkoa wa huo,Godfrey Zambi wakati akizungumza na wakazi wa Lindi alipokuwa akifunga kilele cha maonyesho ya biashara ya wajasiliamali wadogo wa viwanda (SIDO) kanda ya kusini mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa mpira wa Ilulu uliopo mkoani humo,maenyesho hayo yalikuwa ya siku nne ambapo kilele chake kimefanyika jana.
Alisema kuwa iwapo bidhaa zinazozalishwa na wafanyabiashara hao zikiwa na viwango vinavyotakiwa katika soko la kimataifa itawasaidia kuweza kuuza bidhaa zao kwa uharisi zaidi na pia kuweza na wigo mpana wa kibiashara kwa kutangaza bidhaa za tanzania.
Alisema sifa kubwa kwa wafanyabishara duniani ni pale wanapozalisha bidhaa zenye viwango maana hata zinapopelekwa katika soko la kimataifa inakuwa ni rahisi kuuza na hata bei pia uuzwa kwa bei kubwa ukilinganisha na bidhaa yenye viwango hafifu.
Aidha,Zambi alisema wafanyabiashara hao ni lazima watumie vifungashio nywenye ubora katika kufungasha bidhaa
Mkuu huyo wa mkoa alisema maonyesho hayo iwe ni fursa pekee kwa wafanyabiashara hao kubadilishana uzowefu ambapo baada ya hapo watakuwa wamejitangaza kupitia bidhaa zao na wataendelea kutengeneza bidhaa bora zitakazoingia kwenye soko la kimataifa na kuweza kuitangaza nchi.
Zambi alisema njia pekee ya kuweza kutambulika katika soko la kimatifa kwa kuitangaza bidhaa ya kitanzania ni lazima wajasilimali hao wawe katika makundi ili iwe rahisi kuwatambua na mamlaka zinazohusika na masuala ya bishara kama vile mamlaka ya chakula na dawa(TFDA) na shirika la viwango Tanzania(TBS)
”Napenda kutoa wito kwa wajasiliamali wa hapa Lindi lakini wote ambao wamefika kushiriki kwenye maonyesho haya ebu tuache kufanya bishara zetu tukiwa ndani majumba yetu tujitokeze kwenye maonyesho kama haya ili hata serikali iwatumbuwe na kuwasaidia kwa kuwapa ushauri,”alisema Zambi
Kwa upande wake meneja masoko shirika la viwanda vidogo (SIDO) Taitas Kialuzi alisema lengo la maonyesho hayo ni kuwakutanisha wajasiliamali hao ili kwa pamoja waweze kubadilishana uzowefu na ujuzi katika kutengeneza bidhaa hasa bidhaa zenye ubora.
Alisema jumla ya wajasiliamali 175 kutoka mikoa mbalimbali nchini wamejitokeza kuja kwenye maonyesho hao na kwamba baadhi ya mikoa ambayo imefika kushiriki maonyesho hayo ni Morogoro,Dar es salaamu,Singida,Mtwara.Lindi, Mbeya,Mwanza, Dodoma na Ruvuma.
….alisema shirika la SIDO litaendelea kuwakutanisha wajasiliamali ili kuwajengea uwezo katika kutangaza bidhaa zao na kuwashauri kuwa na bidhaa bora ambazo hata zitaweza kuonekana kwenye soko la kimataifa.
Post a Comment