Ukiachana na Wachezaji ambao ni majeruhi mpaka sasa licha ya Kuonekana kuanza kuwa fiti Amis Tambwe, Donald Ngoma na Thaban Kamusoko Yanga imeanza kuingia hofu kuelekea Pambano kati yake na Simba kutokana na wachezaji wake muhimu kuwa na Kadi mbili za njano.
Kelvin Yondani, Juma Abdul na Raphael Daudi hawa wote wanakadi mbili za njano na ikitokea wamepata kadi za njano katika mchezo dhidi ya Stand United Chama la wana kutoka Shinyanga Jumapili hii Oktoba 22 basi itawakosa wachezaji hao muhimu katika mchezo dhidi ya Simba
Wachezaji hao walipata kadi hizo za Pili za Njano wakati Yanga ikicheza dhidi ya Kagera Sugar wanankurunkumbi Huku Yanga ikiibuka na Ushindi wa bao 2 kwa 1 mabao ya Chirwa na Ibrahim Aji Migomba.
Chanzo-kwataunit.com
Post a Comment