0



Kaimu  Mkuu  wa  mkoa  wa  Lindi  Shaibu  Ndemanga  amewataka vijana  kutumia  vizuri mikopo kwa kubuni shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawasaidia kuondokana na  umasikini na kuacha  tabia  ya kutumia mikopo  hiyo kwa kuwarubuni wanafunzi kimapenzi na kuwapa mimba .

  Kauli  hiyo ameitoa  jana  alipokuwa akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana zaidi ya 150 kutoka mkoani humo,mafunzo ambayo yanalengo la kuwajengea uwezo wajasiria katika kubuni miradi ya kiuchumi kwa vijana mafunzo hayo yanaratibiwa na Taasisi ya ujasiriamali na ushindani Tanzania (TECC) chini ya mradi wake wa mwaka mmoja uitwao “Kijana Jiajiri” ,ambapo yalifanyika katika ukumbi wa Kagwa mjini Lindi.

  Ndemanga  alisema iwapo vijana wakitumia  vyema mikopo ambayo wamekuwa wakipewa na taasisi za fedha kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi wataweza kuinuka kiuchumi na kondokana  na  umaskini baada  ya  kuwa  na  shughuli za kufanya  na  kuepukana  na  kukijiingiza katika mambo yasiyo na maadili katika jamii.

  Alisema wapo vijana ambao wamekuwa wakifanikiwa kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha lakini baadhi yao wamekuwa wakitumia mikopo hiyo vibaya kwa kuwarubuni wanafunzi kimapenzi na kuwapa mimba jambo ambalo lengo la mikopo hiyo limekuwa likipotea na vijana hao kuendelea kuwa masikini wa vipato.

   Ndemanga aliongeza kuwa  iwapo vijana  wataanzisha shughuli za kiuchumi kama vile viwanda vidogovidogo kwenye maeneo yao vitawasaidia kuweza kuinuka kiuchumia na kutimiza adhima ya serikali ya John Magufuli ya uchumi wa viwanda.

“Matarajio yangu kuwa baada ya mafunzo haya kumalizika mtakwenda katika ngazi ya kijiji na kata kukutana na vijana wengine ambao hajawafanikiwa kupata mafunzo haya muhimu mkawapa kile mlichojifundisha ili na wao wawe na ustadi kama ninyi tunachotaka ni kila kijana ajekuwa mjasiriamali mzuri katika miradi ya kuichumi,”alisema Ndemanga.

Kwa upande wake mkurugenzi wa baraza la uwezeshaji kiuchumi kitaifa,Beng’hi Issa alisema vijana ni nguvu kazi ya taifa hivyo ni lazima watumie fursa wanayopata kwa kutumia vema mikopo ya ujasiriamali kwa kujiendeleza kiuchumi.

Issa alisema baraza la uwezeshaji kiuchumi kitaifa litaendelea kufungua wigo wa kuwakutanisha vijana ili kwa pamoja kuwajengea mazingira rafiki ya kuwapa uwezo wa kubuni miradi ya ujasiriamali itakayowawezesha kujenga uchumi imara ndani ya maisha yao na taifa kwa ujmla.

“Tunawaomba vijana waache kujiona kama wanyonge katika kukuza uchumi wa taifa bali wawe chachu ya maendeleo kwa kujishughulisha katika shughuli za kuichumi kwa kubuni miradi ya maendeleo kupitia mikopo wanayopata kutoka kwenye taasisi zafedha nchini,”alisema Issa/

  Akitoa neno kwa vijana hao mkuu wa chuo cha VETA mkoani Lindi,Samuel Nando alisema kundi kubwa la vijana katika mikoa ya Lindi na Mtwara bado hawajawa na mwamko wa kujiunga kwenye vyuo vya VETA kwa ajili ya kujifunza masomo ya stadi za kazi ikiwemo seremala,ufundi wa magari,ushonaji,ubunifu wa miradi na uashi.

  Alisema kutokana na hali hiyo ya kuwapo kwa mwamko mdogo kwa vijana wa mikoa ya Lindi na Mtwara kujiunga na VETA vyuo hivyo vinaamua kuwachukua vijana kutoka katika mikoa ya Kaskazini ili wajekusoma kwenye hivyo ili vyuo hivi visijiendeshe kiharasa.

  “Tunalazimika kuwachukua vijana wa mikoa ya kaskazini ambako vijana wa huko ndio wanaonekana kuwa na mwamko wa kutaka kusoma katika vyuo hivi vya VETA maana kama tusipofanya hivi vyuo vyetu tunakuwa tukiviendesha kwa hasara kwa sababu vijana wa huku bado hawana mwamko ingawa wapo wengi sana , “alisema Nando

 Naye mshiriki wa mafunzo hayo ambaye ni kijana Catherine Mremi alisema baada ya mafunzo hayo kumalizika anatarajia kuwa na ustadi mkubwa wa kubuni miradi ya ujasiriamali kwa vile anakuwa tayari ameshapata ujuzi wa masuala ya ujasiriamali.
  Alisema anawaasa vijana ambao wamekuwa wakipata mikopo kutoka katika taasisi za fedha kuitumia vema mikopo hiyo kwa kufanyia shughuli za kuichumi ambazo zinalenga kuwainua kuichumi badala ya kufanyia mambo ya hanasa ambapo mwisho wa siku bado wanatajikuta wakiendelea kubaki nyuma kiuchumi.

 “Ndoto yangu ni kuwa mjasiriamali mkubwa hapa mkoani Lindi hivyo nimefurahi sana kuwa mmoja wa sehemu ya vijana wanaopata mafunzo haya leo na naamini baada ya kumaliza mafunzo na kama nikipata mkopo nitautumia vema kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi,”alisema Mremi

   Alisema kwa sasa vijana wengi wamekuwa wakifanikiwa kupata mikopo lakini kutoka na kuweka mbele starehe za kianasa wanajikuta mikopo wanayochukua wakishindwa kurejesha lakini inachangia na ukosefu wa elimu kama hii

Post a Comment

 
Top