0
           VIFO LINDI
Imeelezwa kuwa upungufu wa watoa huduma za afya,ukosefu wa maji ikiwemo umbali wa zahanati na vituo vya afya pamoja na vituo vingi vya afya kutotoa huduma za upasuaji ni baadhi ya sababu zinazochangia kuongezeka kwa vifo vya akina mama na watoto katika mkoa wa Lindi ambapo jumla ya akina mama 36 na watoto 70 wamepoteza maisha katika kipindi cha januari hadi septemba mwaka huu
Akifungua kikao cha siku tatu kwa ajili ya kupanga mipango mkakati ya kuboresha huduma ikiwemo afya ya mama na Mtoto kwa waganga wakuu wa wilaya,watoa huduma za afya pamoja na asasi zisizo za kiserikali,Mkuu wa wilaya ya Lindi ,Shaibu Ndemanga amemuagiza mganga mkuu wa mkoa wa lindi kusimamia watoa huduma kutoa huduma kwa kuzingatia weledi kwa wagonjwa ili kupunguza vifo pindi wanapotoa huduma
Akitoa taarifa ya utoaji huduma katika mkoa wa Lindi,Mganga mkuu wa mkoa wa Lindi alibainisha kuwa pamoja na changamoto mbalimbali zinazokabili utoaji wa huduma alieleza kuwa mkoa huo wenye vituo vya afya 19 hakuna hata kimoja kinachotoa huduma za upasuaji hali ambayo inasababisha wajawazito wenye uzazi pingamizi kuchelewa kufika katika hospital za wilaya na mkoa
Awali akitoa takwimu za vifo vya akina mama na watoto vilivyotokea mwaka huu,Mratibu wa huduma za akina mama na watoto mkoa wa Lindi ,Zainab Mathradas pamoja na mganga mkuu wilaya ya Ruangwa na Katibu wa afya wilaya kilwa walibainisha utatuzi wa changamoto hizo ikiwa na kutoa wito kwa wajawazito
Na Mwandishi wetu Abdulaziz Ahmed – Lindi

Post a Comment

 
Top