Jukwaa la radio Mashujaa fm 89.3 likirusha matangazo ya moja kwa moja oktoba 15 kwenye uzinduzi wa kituo hicho kutoka uwanja wa michezo wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi
Mkuu wa wilaya ya Liwale,Mhe. Sarah Chiwamba akizungumza kwenye uzinduzi wa radio Mashujaa fm oktoba 15 kwenye uwanja wa michezo wa wilaya ya Liwale
Mashujaa Group Limited ambao wamiliki wa kituo cha radio Mashujaa fm yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam imekuzindua kituo chake kilichopo kijiji cha Makonji kata ya Nangando katika wilaya ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Radio Mashujaa fm ina miaka mine toka kianze kirusha matangazo yake mkoani Lindi awali kituo hicho kiliweza kusikika mkoani Lindi katika maeneo mbalimbali ikiwa Lindi mjini,Lindi vijijini na baadhi ya maeneo mkoani Mtwara.
Baada ya mamlaka ya mawasiliano kujiridhisha imeridhia kutoa ruhusa kwa radio Mashujaa fm kusika maeneo ya wilaya ya Nachingwea,Liwale pamoja na wilaya ya Kilwa.
Awali akisoma lisala Meneja wa Mashujaa fm,Zakia Gasper alisema kituo cha Mashujaa fm ndio kituo cha kwanza kusikika Liwale ambapo itasaidia kuleta changamoto mbalimbali za kiuchumi na kuwa chanzo cha ajira kwa vijana wa wilaya hii wenye taalum ya uandishi wa habari na utangazaji.
Pia amemuomba mkurugenzi wa halmashauri na uongozi wa wilaya kuweza kutoa ushirikiano kwa timu yote ya Mashujaa fm pale watakapofuatilia mashuala mbalimbali yanayowahusu wananchi kuwa tayari kuyajibia na amemuomba mkurugenzi kutoa ruhusa kwa wakuu wa idara kujibia mambo yaliyo ndani ya idara yao kuweza kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili kuweza kuijenga wilaya.
Kwa upande wake mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya,mhe. Sarah Chiwamba alisema kupita kituo cha Mashujaa fm wananchi wataweza kuvitangaza vivutio mbalimbali vilivyopo Liwale na amewaomba wananchi kuweza kutoa ushirikiano na kituo cha Mashujaa fm.
Mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi kuweza kutumia kituo hicho cha radio kwa maendeleo ikiwa kuongea maneno ya ukweli na kutangaza amani ili kuijenga wilaya na aliongeza kusema kuwa wananchi wasitumie mwanya wa kituo hicho kuwa sehemu ya kupoteza amani au sehemu ya malumbano ya kisiasa.
Wageni waalikwa na viongozi mbalimbali mbalimbali walioudhulia kwenye uzinduzi wa radio Mashujaa fm wilayani Liwale
Meneja wa Mashujaa fm,Zakia Gasper akisoma lisala
Wakazi wa wilaya ya Liwale wakiwa wanafuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi wa radio Mashujaa fm uliofanyika katika uwanja wa wilaya ya Liwale
Wakazi wa wilaya ya Liwale wakiwa wanafuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi wa radio Mashujaa fm uliofanyika katika uwanja wa wilaya ya Liwale
Burudani nayo kutoka kwa wakazi wa Liwale ziliweza kukonga roho za wananchi
KUANGALIA SHOW YOTE VIDEO IPO >>>HAPA<<<
Post a Comment