0
MANISPAA ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imetiliana saini  mkataba  wa sh.bilioni 5.56 na kampuni ya ukandarasi  ya  CRJE  ya nchini China  kwa ajili ya  kuanza ujenzi wa kiwanda  cha kuchakata taka kuwa mbolea aina ya mboji .

Kiwanda hicho  ambacho kitakuwa na uwezo wa kuchakata  takaka tani  tano (5) hadi 100 kwa siku kitajengwa katika eneo la Mabwepande.

Akizungumza wakati wa hafla ya utilianaji saini, Dar es Salaam,  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta amesema kuwa kiwanda hicho ambacho ujenzi wake unaanza rasmi leo kitakuwa na uwezo wa kuchakata taka ngumu na laini kuwa  mbolea aina ya mboji.

Amesema manispaa  imekuwa ikitumia kati ya sh.milioni 500 hadi 600 kwa mwezi  kugharamia uzoaji wa taka ambazo hizo taka hazizalishi chochote.

Sitta amesema Manispaa ya Kinondoni  inazalisha   tani 22,000 kwa siku hivyo kutumia fedha nyingi kuwalipa makandarasi.

Amesema  zaidi ya wananchi 1000 wanatarajiwa kunufaika na ajira kupitia kiwanda hicho.

Aidha amesema  hatua hiyo kubwa ya kuitikia sera ya taifa ya kuelekea  uchumi wa viwanda na kinondoni tunakuwa kuzalisha mbolea aina ya mboji ambayo haina madhara  katika udongo ukilinganisha na mbolea za kemikali,”.

 Meneja wa Kanda  wa kampuni ya CRJE,  Bai Haochen amesema, ujenzi wa kiwanda hicho unaweza kuchukua muda wa miezi 12  hadi 18. 
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta na Meneja wa Kanda  wa kampuni ya CRJE,  Bai Haochen wakitiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka na kuwa mbolea leo jijini Dar es Salaam.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta akizungumza na waandishi wa habari juu ya makubaliano na kampuni ya ukandarasi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kuwa mbolea leo jijini Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta na Meneja wa Kanda  wa kampuni ya CRJE,  Bai Haochen wakibadilishana hati za makubaliono leo jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top