0

Naibu waziri wa maendeleo ya jamii jinsia  wazee na  watoto Hamisi Kigwangala ameitaka  Halmashauri ya Manspaa ya Lindi  kutumia fedha milioni hamsini zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa zahanati ya kineg'ene kama  ilivyo  kusudiwa.

 Ametoa kauli hiyo majuzi alipotembelea katika zahanati ya kineng'ne mjini  hapo  na kuona jitihada za wananchi wa kata hiyo ya kukarabati zahanati ambayo inatarajiwa kuwa kituo cha afya bada ya kukizi vigezo vya wizara ya afya

Kigwangala amesema ili zahanati hiyo iwe kituo cha afya ni lazima majengo muhimu yajengwe ikiwemo chumba cha upasuaji, mahabara ,chumba cha kujifungulia na wodi ya kulala akina mama baada ya kujifungu hivyo ni muhimu fedha ambazo wamezipato kutoka serikari kuu kuzitumia kwa matumizi tarajiwa 

Akaongeza kuwa ipo tabia ya baadhi ya wakurugezi kubadilisha matumizi katika fedha inayopangwa kwa shuguri fulani lakini katika hili ili kufikia lengo la kuifanya zahanati hiyo ya kineng'ene kuwa kituo cha afya ni lazima majengo hayo muhimu yajengwe ndipo zahanati hiyo itapandisha adhi kuwa kituo cha afya

Ukarabati wa zahanati hiyo ambao utagarimu zaidi ya shilingi milioni mia 118 tayari  serikari imetenga  kiasi cha milioni 50 ambazo milioni mia 350 zitaenda kujenga miundombinu na milioni 150 zitakazobaki ni kwa ajili ya kununua vifaaa tiba ambao zahanati hiyo unatarajiwa  kuwanufaisha wakazi zaidi ya 5270 ambao wanaishi katika kata hiyo na wanapata huduma katika zahanati hiyo

 Nae afisa mtendaji wa kata ya kineng'ene Salumu Abdalah amesema kwa kutambua kero wanayoipata wakazi wa kata hiyo tayari wao wenyewe wamechangia kiasi cha shilingi milioni sita ambayo imetokana na mradi wa maji uliopo katika kata hiyo  na kuweza kununua matofari pamoja na kufanya usafi katika eneo ambalo linatarajiwa kujenga majengo hayo

Na kuongeza kuwa kilichowakwamisha mpaka kufikia wakati huu kutokuanza kwa ujenzi wa baadhi ya majengo tarajiwa ni udogo wa eneo wanalo limiliki ambapo kwasasa mbunge wa jimbo hilo slemani kaunje amejitolea kuongeza eneo ambalo lipo karibu na zahanati hiyo ili kuendelea na ujenzi na sasa kinachosubiliwa ni wataalamu kuja kupima na kuhakiki eneo hilo


Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi Agnes Mnali amesema zahanati hiyo inaudumia mitaa minne ambayo ni mchochoro, nanembo, mtutu na mmukule pamoja na mitaa jirani kama vile mkanga, jangwani na mtange huku ukubwa wa tatizo  la kutokuwa na majengo pamoja na baadhi ya vifaa tiba  katika zahanati hiyo upelekea  kushindwa kuwalaza wagonjwa ambao wamekwenda kupata huduma katika zahanati hiyo na kulazimika kuwapa rufaa ili wakatibiwe hospitari ya rufaha sokoine  

Post a Comment

 
Top