0
Nyumba 1,500 zimeharibiwa na moto huoHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionNyumba 1,500 zimeharibiwa na moto huo
Maeneo ya jimbo la California ambayo hukuza mizabibu yameathiriwa na moto mkubwa ambao unaenea kwa kasi sana na kusababisha vifo vya watu 10.
Mamia ya watu wamehamishwa makwao na inakadiriwa kwamba zaidi ya nyumba 1,500 zimeharibiwa na moto huo.
Watu saba waliuawa katika wilaya ya Sonoma, maafisa wamesema.
Watu zaidi ya 20,000 wamekimbia wilaya za Napa, Sonoma na Yuba baada ya moto mbaya zaidi wa nyika kuzuka maeneo hayo.
Gavana wa jimbo la California ametangaza hali ya dharura.
NapaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionMoto unawaka katika maeneo 14 katika wilaya nane za kaskazini mwa California
"Moto huu umeharibu sana nyumba na miundo mbinu mingine na unaendelea kutishia maelfu ya nyumba, jambo ambalo limesababisha haja ya kuwahamisha maelfu ya watu," taarifa ya gavana imesema.
Kando na watu waliofariki Sonoma, wengine wawili wamefariki Napa na mwingine mmoja Mendocino.
Inaarifiwa kwamba kuna majeruhi wengine zaidi na wapo pia watu ambao bado hawajulikani waliko.
Map locator
Marian Williams mkazi wa Kenwood, Sonoma amesema yeye na majirani zake waliutoroka moto huo kwa msafara wa magari.
"Ni moto mkubwa ajabu, hatujawahi kuona moto kama huo," ameambia shirika la utangazaji la NBC.
Mkuu wa idara ya misitu na kinga dhidi ya moto California Kim Pimlott, amesema nyumba 1,500 kufikia sasa zimeharibiwa.
Chanzo cha moto huo uliozuka Jumapili usiku bado hakijabainika.
Mkuu wa kukabiliana na moto wilaya ya Napa amesema hali ya kiangazi katika eneo hilo inaathiri juhudi za kuukabili moto huo na kwamba wameomba usaidizi kutoka wilaya nyingine jirani.
Wafanyakazi wengi wa mashamba hayo ya mizabibu wamehamishiwa maeneo salama kwa ndege.
Nyumba na magari yaliyoharibiwaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Moto huo unaenea kwa kasi sana kutokana na upepo mkali, ukavu na joto kali.
Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa imetoa tahadhari eneo lote la San Francisco na kusema "moto ukizuka basi kuna uwezekano utaenea kwa kasi sana".
Mmiliki mmoja wa mizabibu aliambia gazeti la LA Times kwamba anaamini shamba lake limeharibiwa baada yake na familia yake kukimbilia usalama Jumapili.
"Upepo ulikuwa unazuka na kufifia. Ndimi za moto zilituzingira," amesema Ken Moholt-Siebert.
Maafisa wa kuzima moto California wanakadiria kwamba eka 70,000 zimeteketezwa na moto huo.
Jimbo la California limekuwa likiathiriwa na moto miezi ya karibuni.
Septemba moto mkubwa uliathiri jiji la Los Angeles.

Post a Comment

 
Top