Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es
Salaam inatarajia kuanza kusikiliza kesi ya mauaji ya bila kukusudia
inayomkabili Mwigizaji Elizabeth Michael maarufu kama Lulu October 19, 2017.
Lulu anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kumuua Msanii mwenzake, Steven
Kanumba bila kukusudia, kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za
Adhabu (PC), April 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza
Vatican.
Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji ya bila kukusudia
iliyotolewa na Mahakama Kuu, kesi ya Lulu itaanza kusikilizwa siku hiyo
ya October 19, 2017 mbele ya Jaji Sam Rumanyika.
February 18, 2014 akisomewa maelezo ya awali (PH) alikiri Mahakamani
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kanumba na pia kuwa kulikuwepo na
ugomvi baina yao siku ya tukio la kifo cha Mwigizaji huyo.
Lulu aliachiwa kwa dhamana January 29, 2013 baada ya kesi hiyo
kubadilishwa hati ya mashtaka kutoka kwenye kesi ya mauaji ya bila
kukusudia ambapo badiliko hilo lilimpa nafasi ya kupata dhamana.
Katika kesi ya msingi namba 125 ya mwaka 2012, inadaiwa kuwa April 7,
2012 Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, Lulu alimuua Kanumba bila
kukusudia.
Post a Comment